Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wamelalamikia ahadi zisizotekelezeka za kukamilishwa kwa mradi wa Umeme wa REA katika vijiji vyao bila mafanikio jambo linalosababisha maswali kwa wananchi.
Katika Mkutano wa baraza la madiwani wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 baadhi ya madiwani hao akiwemo Roida Wandelage,Innocent Gwivaha na Isaya Myamba wamesema ahadi za kuwashwa kwa umeme huo hazitekelezeki kwenye maeneo mengi huku transfoma zinapoungua kwenye maeneo yenye umeme kubadilishwa kunachukua muda mrefu.
Akitolea ufafanuzi wa hoja za madiwani hao Msimamizi wa Miradi ya REA toka shirika la umeme Tanesco wilaya ya Njombe Bwana Nathanael Laizer amesema hatua mbalimbali za kufikisha umeme kwenye vijiji zinaendelea kwa kuwasimamia wakandarasi kupitia REA.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilayaya Njombe Bwana Melkizedeck Kabelege ameagiza Tanesco kuwasimamia wakandarasi ili wananchi wapate umeme.
Serikali imekusudia kufikisha umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo 2025 kupitia wakala wa umeme vijijini REA na hivyo ili kufanikisha azma hiyo ni lazima usimamizi wa karibu kufanyika na mamlaka husika.
0 Comments