Header Ads Widget

WAZEE KIGOMA WALIA KUTELEKEZWA, KUNYANYASWA

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma


WAZEE mkoani Kigoma wametoa ushuhuda wao wa mateso na manyanyaso wanayoyapata yanayofanya wengi wao kuishi maisha yasiyo na furaha hivyo kuiomba serikali na familia mbalimbali kusimamia kwa karibu matunzo na mahitaji ya wazee.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Endeleza Wazee Kigoma (EWAKI), Cotilda Kokupima alisema hayo kati ahafla ya harambee ya ujenzi wa kituo cha kuhifadhia na kusaidia wazee kwenye kata ya Nyumbigwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma.




Kokupima alisema kuwa katika utafiti uliofanywa na taasisi hiyo ambao umefikia wazo la kujengwa kwa kituo hicho unaonyesha kuwa wazee wengi wametelekezwa na watoto wao wa kuwazaa na familia zao hivyo wengi kukimbilia mtaani na kuishia kulala kwenye vibaraza vya mitaa na majumba mabovu kama sehemu za faraja kwao.

 


“Wazee wengine wamegundulika kuwa na watoto ambao ni watumishi wa serikali au taasisi mbalimbali wakiwa na uwezo mkubwa lakini wamewatelekeza wazazi wao na kuwafanya wazee wao kuishi maisha magumu  huku wengine wakikosa huduma muhimu ikiwemo chakula, tunao wazee 64 ambao tunawatafutia namna ya kuweza kupata mahitaji kwani wana hali mbaya ya kupa mahitaji,”Alisema Kokupima.



Akizungumzia ujenzi wa kituo hicho alisema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 kinahitajika kwa ajili ya majengo manane yatakayotumika kutoa huduma ikiwemo jengo ambalo litatumika kwa ajili ya makazi na malazi ya wazee, jengo la kliniki, ofisi za watendaji na jengo la kufanyia mazoezi mbalimbali.




Mmoja wa wazee waliohudhuria hafla hiyo, Gerlad Nkona (65) mtumishi mstaafu wa serikali alisema kuwa wazee wengi wamekuwa kwenye matatizo makubwa kutokana na maisha wanayoishi sasa hata kama wakati wa ujana wao walikuwa na maisha mazuri.



Nkona alisema kuwa wapo wazee wametelekezwa na watoto wao na familia zao na sasa wanaishi mtaani lakini pia hayo yana chanzo chake ikiwemo kutokuwepo kwa mahusiano mazuri na watoto na familia lakini wengi hawajiandai na maisha ya baadaye ya uzeeni.

 


Naye Mzee Abdallah Ndayeza alisema kuwa licha ya wazee wengi kutelekezwa na kukosa matunzo lakini pia wamekuwa hawapati msaada hata wa kiserkakli hasa kwenye matibabu na wazee wengi ambao hawana uwezo kiuchumi wamekuwa wakihangaika namna ya kupata matibabu.




Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa wilaya Kasulu,Kanali Isack Mwakisu alisema kuwa kuanzishwa kwa mpango huo wa kuhifadhi wazee kunakofanywa na taasisi ya EWAKI kunatokana na juhudi kubwa ya serikali ikiwemo upatikanaji wa eneo husika na misaada mbalimbali ikiwemo ya kifedha kwa taasisi hiyo.

 


Kanali Mwakisu ambaye alikuwa mwenyekiti wa kusimamia harambee hiyo alisema kuwa serikali kupitia sheria na sera ya wazee inayotekelezwa ni wazara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto inasimamia kwa karibu kuona wazee wanapata mahitaji muhimu na wanapewa kipaumbele kwenye mambo mbalimbali.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI