Header Ads Widget

TAASISI YA SAUTI YA SHANGAZI YATOA ELIMU YA KUJITAMBUA KWA WANAFUNZI MBINGA.

 



Na Amon Mtega,Mbinga.


 TAASISI  isiyo ya Kiserikali (NGO'S) ya Mwanamke kwa Maendeleo endelevu (WSDO)  kupitia Mradi wa SAUTI YA SHANGAZI Ndugu imetembelea katika shule ya Sekondari ya Wasichana (Mbinga Girls) Mkoani Ruvuma kisha toa elimu ya kujitambua kwa wanafunzi hao.


 Akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Mary Mwenisongole amesema kupitia Taasisi hiy wamekuwa wakipita kutoa elimu ya Uzalendo, kujitambua dhidi ya Rushwa, Ukatili wa Kijinsia na kuwakumbusha umuhimu wa kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto na malengo yao.


 Mwenisongole ambaye ameambatana na mtumishi kutoka ofisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU)katika Wilaya ya Mbinga Blandina Hamis  pamoja na Bosco Mkandawile akizungumza na wanafunzi hao amesema kuwa baadhi ya wanafunzi  wa kike wamekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao kielimu kutokana na kutokuwa na Elimu ya kujitambua.



Mkurugenzi huyo amewaambia wanafunzi huo kuwa kuanzia sasa wawe wanajitambua na kuweza kuvishinda vishawishi mbalimbali ambavyo vimekuwa vikiwafanya baadhi kushindwa kumudu masomo darasani.


Pia Mwenisongole mkurugenzi wa Taasisi hiyo amemshuku Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia  Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu huku akiwashukuru pia wabunge wa majimbo mawili Mbinga mjini Jonas Mbunda na Mbinga Vijijini Benaya Kapinga kwa kufanya  kazi za kiwakilishi wanazotumwa na Wananchi wao ikiwemo kutambua umuhimu wa Elimu.


Aidha Taasisi hiyo imetoa mahitaji ya Vitu mbalimbali kwa Wanafunzi kama vile taulo za kike, vifaa vya Masomo (Counter book) pamoja na vifaa vya Michezo ikiwemo mipira miwili.



Kwa upande wake Afisa kutoka Ofisi ya Takukuru Blandina Hamis ambaye alimwakilisha mkuu wa Takukuru Wilayani Mbinga Frederick Msae akitoa Elimu ya kupambana na Rushwa kwa wanafunzi hao amesema kuwa wanatakiwa kuichukia rushwa na kupambana nayo  tangu wakiwa shuleni ili kulifanya taifa siku za mbele kuwa na watu wenye uzalendo.


Blandina akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Takukuru wametoa msaada wa kumsomesha mmoja wa wanafunzi wa kidato cha kwanza jina limehifadhiwa ambaye anatokea katika mazingira magumu kutokana na kufiwa na wazazi wake wote .



"Wanafunzi mimi mkuu wangu kanituma kasema licha ya kutoa elimu ya Rushwa lakini nihakikishe tunapata mwanafunzi mmoja anayetokea mazingira hatarishi ili asomeshwe ,wote mmempendekeza huyu na mmemuibua wenyewe kuwa anamazingira hatarishi na sisi tumekubaliana nanyi na atasomeshwa "amesema Blandina Hamisi Afisa wa Takukuru.


Naye mmoja wa Wanafunzi Nuru Selemani amesema Elimu waliyoipata kupitia Taasisi hiyo wataifanyia kazi ili k


uyafikia malengo yaliyokusudiwa kwenye maisha yao.

        

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI