Header Ads Widget

VIJIJI 32 VYAPATA MAJI YA BOMBA MUSOMA VIJIJINI




Na Shomari Binda-Musoma


VIJIJI 32 katika jimbo la Musoma vijijini tayari vimepata maji ya bomba kutoka ziwa victoria huku vingine vikiendelea kufikiwa na huduma hiyo.


Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini,Profesa Sospeter Muhongo,amesema hiyo ni hatua kubwa iliyofanywa na serikali katika kuwafikishia huduma wananchi.


Amesema katika kipindi kifupi kazi kubwa imefanyika kuwafikishia wananchi maji hasa kwenye maeneo ambayo yalikuwa hayana maji.


Muhongo amesema vijiji vyote 68 vilivyopo jimbo la Musoma vijijini vina miradi ya maji inayoendelea ikiwemo ya visima na kutoka ziwa victoria.



Amesema vijijini 15 vimepatiwa fedha za miradi ya maji na kazi inaendelea kwa kasi ili kuweza kuwafikishia wananchi maji kwenye maeneo yao.



Mbunge huyo amedai kuwa vijiji 12 vinavyosimamiwa na Ruwasa na 7 vilivyo chini ya Muwasa vinakamilishiwa usanifu na vipo kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024.


" Tunaishukuri sana serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais,Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa kutupatia miradi mingi ya  maji ambayo inakwenda kwa kasi.



" Usimamizi wa Ruwasa na Muwasa ni mzuri na miradi yetu yote inakwenda vizuri ya maji kutoka ziwa victoria na ile ya visima",amesema Muhongo.


Amesema maji ni uchumi na maendeleo hivyo wananchi wanapaswa kulinda na kutunza miundombinu yake ili iweze kudumu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI