Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali ya awamu ya sita imeahidi kuendelea kushughulikia maslahi ya wafanyakazi nchini ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza tija kazini.
Katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zinazofanyika kwa siku mbili mkoani Njombe kutokana na mwingiliano wa ujio wa mwenge wa uhuru mkoani hapa katibu tawala mkoa Bi.Judica Omary kwa niaba ya mkuu wa mkoa wakati akizungumza na wafanyakazi amesema tayari changamoto zilizokuwa zikilalamikiwa zimeanza kushughulikiwa na zitaendelea kutatuliwa.
Awali mwenyekiti wa shirikisho la wafanyakazi nchini TUCTA Mkoa wa Njombe Dokta Mashaka Kisulila ambao ni waandaaji wa sherehe hizo amesema siku ya wafanyakazi duniani ilikuja baada ya manyanyaso ya wafanyakazi ambao walikuwa wakilalamikia maslahi duni pamoja na makazi na hivyo kama TUCTA wataendelea kuwapigania.
Sherehe hizo zilizo husisha utoaji zawadi kwa wafanyakazi hodari zimefanyika kimkoa mjini Njombe ambapo baadhi ya wafanyakazi waliopata tuzo hizo akiwemo Francisco Haule na Sarafina Kaduma wameonesha furaha yao baada ya kupata zawadi hizo huku wakiwataka ambao hawajapata kuzingatia nidhamu,ubunifu pamoja na kuzingatia sheria za kazi.
Siku ya pili ya maadhimisho hayo katika mkoa wa Njombe inafanyika Mei Mosi ikihusisha kusikiliza hotuba ya mkuu wa mkoa pamoja na hotuba ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan atakapokuwa mkoani Morogoro kwenye sherehe za Mei mosi Kitaifa.
0 Comments