WANANCHI wa tarafa
ya Ismani wilaya ya
Iringa mkoani Iringa
wamesema watashirikiana na jeshi la
polisi wilaya ya Iringa kuwafichua
watu wanaojihusisha na wizi
wa mifugo ili
sheria ichukue mkondo
wake .
Wakizungumza leo mbele ya mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) Bernad Samala wananchi hao walisema kuwa vimeanza kuibuka vitendo vya wizi wa mifugo katika tarafa yao na wahusika hawatoki mbali na tarafa hiyo na ni watu ambao wanatoka ndani ya tarafa hiyo na baadhi yao majina yao wanayo.
Hivyo waliomba kupitia
vikao vyao vya
vijiji ,kata na tarafa
wataendelea kuwafichua wezi hao kupitia vikao
hivyo ambavyo pia wamekwisha unda
kanda maalum ya
kuthibiti wizi wa mifugo
ambayo itajumuisha kata sita
katika tarafa hiyo ya Isimani .
Mwenyekiti wa
wafugaji kanda ya Isimani
Baraka Sosopi alisema
kuwa kupitia mkakatii wao
wa kuunda kanda maalumu ya
kuthibiti wizi wa mifugo
wanaimani kubwa watafanikisha vita dhidi ya
vitendo vya wizi wa
mifugo .
Kwani walisema kuwa wezi
hao wa mifugo wamekuwa
wakijigamba wazi wazi kuwa
hakuna wa kuwafanya
lolote kwani enzi za utawala
wa Magufuli waliishi kwa
hofu kutokana na kubanwa ila sasa wanadai
wapo huru jambo ambalo limekuwa likitishia
usalama wa mifugo yao .
Akizungumza mara baada ya
kikao hicho mkuu wa
polisi wilaya ya Iringa (OCD) Samali alisema
kuwa wao kama jeshi la
polisi wanataka kuona
wafugaji na wananchi wa
wilaya ya Iringa wanaishi kwa uhuru
pasipo kuwepo vitendo
vya vyovyote vinavyotishia
usalama wa rai ana mali
zao .
Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa kupitia kikao
hicho jeshi la polisi linaamini
kuwa vitendo vya wizi wa mifugo na mali za wananchi
katika eneo hilo vitakwenda kwisha .
Hivyo aliwataka wananchi wasiogope kuwataja kwa siri wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ili jeshi la polisi liweze kuwakamata kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
0 Comments