Header Ads Widget

SERIKALI IWALINDE WATOTO WANAOISHI NA KUFANYA KAZI MITAANI

  






Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga. 

Tuungane pamoja na kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani wanalindwa, wanakuwa salama na kupewa haki zao za msingi kama watoto wengine.


Hiyo ni kauli ya Mtaalam wa masuala ya ulinzi na usalama wa watoto (Expert in Child Protection and Safeguarding) Hassan Aufi ambae ni Mwanafunzi wa Shahada ya uzamili ya usatawi wa jamii(open university of Tanzania).


Aufi ambae ana Elimu ya Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Jamii na Ustawi wa Jamii(Bachelor of Arts in Sociology and Social Work)(BA-SSW) na anafanyakazi katika shirika la Amani Centre for street children Jijini Arusha amezungumza na mwandiahi wa makala hii na kuonyesha namna anavyoguswa na kundi hili ambalo limeachwa bila ya kupewa msaada.


Aufi amesema siku ya Kimataifa ya Watoto wanayoishi na kufanya Kazi Mitaani huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Aprili ambapo hutoa fursa kwa 

mamilioni ya watoto wa mtaani kote ulimwenguni na wale wote waliomstari wa mbele katika kupambana ili haki zao zisipuuzwe.


Na ni siku ambayo inatoa fursa kwa mashirika ya kiraia (CSO's) kueneza ufahamu kuhusu matatizo ya watoto wanaoishi na Kufanya kazi mitaani duniani kote jambo ambalo linapingwa kwa maslahi ya watoto hao


Mtaalamu huyo wa masuala ya Ulinzi na usalama wa watoto amesema juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali, Mashirika ya haki za binadamu, na watetezi wa haki za watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani zinaweza kwasaidia watoto hao kuokolewa kutoka mtaani na kurekebishwa tabia zao.


Ingawa jitihada kubwa zinafanyika kila kona ya nchi ikiwemo serikali, mashirika ya haki za binadamu na Asasi za kiraia bado tatizo la watoto hao wanaoishi na kufanya kazi mtaani limekuwa kitendawili na kutokuleta matokeo chanya kwa kundi hilo.


Aufi alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa bila shaka kuna hitajio kubwa la kufanyika tafiti nyingi zitakazo akisi ukubwa wa tatizo la uwepo wa kundi hilo la watoto wa mtaanina njia sahihi ya utatuzi ili kuweza kuwakwamua watoto hao ambao bado haijulikani hatma yao.


Amesema hakika ukifuatilia kwa ukaribu zaidi, wadau wengi wanaofanya kazi na watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani wana mbinu zinazofanana katika kutatua changamoto hiyo ambayo kila uchao bado linaongezeka zaidi kutokana na changamoto na matatizo ya kijamii ambayo kila siku yanakuja na sura mpya tofauti na ile ya mwanzo.


"Lazima tutafakari na kutambua kuwa sababu zilizopelekea kuwepo kwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani kwa miaka ya 1990’s haziwezi kuwa sawa na za nyakati hizi tukibaini tunaweza pata suluhu"alisema Aufi. 


Amesema miongoni mwa sababu ya kuwepo kwa watoto hao wa mtaani baadhi yao huondoka majumbani mwao kutokana na vifo vya wazazi wao na kukumbana na unyanyasaji dhidi yao (kimwili, kingono, kisaikolojia na kutelekezwa) kupelekea.kukimbilia mtaani na kujishughulisha na biashara ndogondogo na baadhi yao wanakuwa wadokozi.


Watoto kama hao tayari wako katika hatari ambayo inaweza kuwafanya kuwa katika hatari zaidi ya vurugu, matumizi ya madawa ya kulevya,wizi,kujihusisha na ngono za utotoni,ajira za utotoni na hata masuala ya afya ya akili.


Imegundulika kuwa watoto wanaoishi mitaani ndio kundi lililotengwa zaidi na wanakosa ulinzi zaidi ulimwenguni, wamewekwa kando,kukosa thamani na zaidi ya hayo hali yao inafanywa kuwa ngumu zaidi kutokana na mitazamo duni ya kijamii ya watoto hao.


Nini kifanyike kunusuru kundi hili,Serikali, Mashirika ya Haki za Binadamu na Asasi za Kiraia (CSO’s) na wadau wengine wa utetezi, haki na ulinzi wa watoto na wanajamii kwa ujumla kuamka na kusimama kidete kutetea haki za watoto hao wanaoishi na kufanya kazi mtaani ili kuwaweka salama. 

 

Amesema kwa upande wa Serikali ishirikiane na wadau, mashirika na taasisi zisizo za kiserikali zinazofanya kazi na watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika kutatua changamoto zinazowakumba watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.


Amesema ipo haja kwa Serikali pia  kuziimarisha  kiuchumi familia masikini na fukara kupitia mfuko wa TASAF ili kuweza kufanya shughuli ndogo ndogo ambazo zitaweza kuwaingizia kipato na kuweza kujikimu vizuri ili kupunguza wimbi la watoto wa mtaani ambao wapo mtaani kwa sababu ya umasikini.


Mbali na hayo watumike  viongozi wa dini na wakitamaduni katika kutoa elimu ya kimalezi na kimaadili zenye lengo la kuwambusha wajibu wao katika uangalizi wa kimalezi kwa watoto wao.


Kwa upande wa Familia Aufi alisema upendo ni jambo jema ambalo likizingatiwa na kuimarishwa misingi ya mizuri ya upendo kwa wanafamilia na wanajamii katika kuishi na watoto walioachwa na ndugu zao baada ya kufariki au kupata maradhi ya kudumu juu ya kuwapa huduma stahiki.


Aufi alisema Mashirika yasiyo ya Kiserikali yashirikiane na Serikali katika kufanya tafiti zinazo akisi tatizo hili ili kuja na mbinu na afya sahihi ya kulitatua tatizo hili unaweza kuwa muarubaini wa kupunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo hilo.


Kauli mbinu ya Siku ya Kimataifa ya Watoto wa mitaani 2023: "Kuwaweka Salama Watoto Waliounganishwa Mtaani

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI