NA HADIJA OMARY
LINDI
Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2023 zimeridhia kuzindua mradi wa ujenzi wa Barabara ya NHC yenye urefu wa km.1.051 kwa kiwango cha lami kijiji cha Kilimahewa kata ya Nachingwea , Tarafa ya Ruangwa Wilayani Ruangwa wenye thamani ya shilingi milioni 562, 196,293.33
Akizungumza na wananchi wa kata ya Nachingwea na wa maeneo jirani walioudhuria ghafala hiyo kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2023 ndugu Abdalla shaibu kaim alisema baada ya kukagua ujenzi huo wa barabara sambamba na kupitia nyaraka zote muhimu mbio za mwenge wa Uhuru umeridhishwa na mradi huo na kwamba upo tayari kuuzindua.
Aidha ndg. Shaibu kaim aliwapongeza wakala wa Barabara mijini na vijijini TARURA kwa kazi mzuri wanayoendelea kuzifanya Nchi mzima.
Kaim pia aliwahasa TARURA kuendelea kufanya kazi hizo kwa uzalendo sambamba na kutanguliza maslahi mapana kwa wabanchi.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge , Meneja TARURA Wilaya ya Ruangwa, Mhandisi Mashaka Martin Nalupi alisema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 wakala wa Barabara vijijini na mijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Ruangwa ilitengewa fedha za maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 3,000,000,000.00 kutoka serikali kuu ikiwa ni fedha za Tozo ya mafuta kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mji wa Ruangwa km 6 ikiwemo na barabara hiyo ya NHC.
Alisema mradi huo ulitekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Ndani M.E AND COMPANY LIMITED ya Jijini Dar es salaam ambapo ujenzi wake ulianza tarehe 08/12/2021 na kukamilika tarehe 14/10/2022 ambao umegharimu kiasi cha milioni 562,196,293.33.
0 Comments