Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU WAZINDUA BARABARA YA LAMI LIHAMBE MAJENGO – MTAMA

 


NA HADIJA OMARY

LINDI…….Wakazi wa halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wameishukuru  serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura kuanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Mtama Lihimba yenye uruefu wa mita 800.

 

Barabara hiyo ambayo ujenzi wake unagharimu kiasi cha shilingi Milioni 469 za mfuko wa jimbo imewekewa jiwe la msingi leo Aprili 11,2023 na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdallah Shaib Kaim.

 

Wakazi hao wakiwemo wa kijiji cha Lihimba,Majengo A na B wamesema barabara hiyo pindi itakapokamilika itawasaidia kusafirisha mazao yao kwa urahisi kutoka mashambani hadi sokoni.

 


 Kwa upande wake  Waziri wa  habari,mawasiliano na teknolojia ya habari ambaye pia ni Mbunge wa jimbo Mtama amesema barabara ya Mtama lihimba itakuwa mkombozi kwa wakazi hao.

 

“huu ni mradi mmoja lakini iko miradi mingi tumeanza kujenga ya barabara za lami, ilikuwa ni ndoto kwa Halmashauri ya mtama kuwa na Barabara za lami kwani tulikuwa na lami moja tuu ya kutoka Mnazi mmoja kwenda masasi”alieleza

Hata hivyo aliwapongeza Suma JKT ambao ndio watekelezaji wa mradi huo kwa kuwa kama halmashauri ni Taasisi ambayo inaitegemewa   katika ujenzi wa miradi mbali mbali.

 

“ Suma JKT imekuwa ni taasisi ambayo kwa sisi wanamtama tumekuwa tunaitegemea ndio tuliowapa kazi ya  ujenzi wa ofisi ya makao makuu ya Halmashauri, wanajenga jengo zuri na wanalikamilisha lakini tumewapa na barabara hii na tunategemea kuwapa na barabara zingine kwa kuwa wao wananidhamu ya kazi na hilo ndilo linalotufanya tuendelee kuwapa kazi” alieleza Waziri Nape

 

Awali akisoma taarifa juu ya ujenzi wa mradi huo wa barabara,Meneja wa Tarura Wilaya ya Lindi Mhandisi Dawson Paschal amesema ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 52 na kwamba inajengwa na Mkandarasi SUMA JKT CONSTUCTION LT.

 

Ameeleza kwamba ujenzi,ulianza  Juni 20 ,2022 na unatarajiwa kukamilika Desemba  20,2023 ambapo  itaunganisha wakazi wa vijiji vya vitatu vya Lihimba,Majengo A na B.

 

Kwa upande wake meneja wa kanda wa ujenzi kutoka SUMA JKT msanifu majengo Luteni Kanali Atupele Mwamfupe  alisema mpaka sasa kazi zilizofanyika ni kusafisha eneo la barabara sambamba na kuchonga barabara mita 800 kuweka kifusi mita za ujazo 3400 na kazi ya kuweka mawe yaliyosagwa mita za ujazo 1200.

“kazi ambazo hazijafanyika mpaka sasa ni kujenga mifereji ya zege, alama za barabarani, ujenzi wa boks la kalavati moja pamoja na kuweka tabaka mbili za lami” alisema Mwamfupe

 

Alisema kwa kazi hizo zilizobaki ni matarajio yake kukamilisha mradi huo kabla ya muda uliopangwa.

 

Nae,Mkimbiza mwenge Kitaifa 2023 Adallah Shaib Kaim amewahimiza wasimamizi wa mradi ambao ni Tarura kumsimamia vyema mkandarasi ili aweze kukamilisha barabara hiyo kwa wakati ulipangwa kwenye mkataba.

Aidha,kwa halmashauri ya Mtama mwenge wa uhuru umezindua mfumo wa Tehama hospitali ya Nyangao,utoaji wa huduma za lishe shule ya msingi Mbalala,umeweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa shule ya msingi Songambele(Nyengedi),uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa tanki la maji Mtama.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI