Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wananchi mkoani Njombe wametakiwa kujiridhisha na mashirika yanayofanya kazi katika maeneo yao ili kukabiliana na matendo ya mmomonyoko wa maadili unaosababishwa na mashirika hayo kwa kutoa elimu zisizofaa kwa vijana na watoto.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa mkutano mkuu wa wazazi taifa CCM mkoa wa Njombe anayewakilisha wilaya ya Wanging'ombe Belshaza Mhanga wakati akizungumza na waaumini wa kanisa la KKKT usharika wa Mambegu uliopo kata ya Luduga wilayani Wanging'ombe katika ibada maalumu ya changizo la ujenzi wa nyumba ya mkuu wa jimbo,ambapo amewataka kujiridhisha na mashirika hayo namna yanavyofanya kazi badala ya kukimbilia kupokea misaada pekee.
Mjumbe huyo wa mkutano mkuu wa wazazi taifa amewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanasaidiana na wazazi kuwalea watoto na vijana katika malezi ya kidini ili kuwaepusha na makundi yasiyofaa.
Aidha Mhanga amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu kwani bila hivyo wataishia kuwa tegemezi na kujiunga na makundi yasiyofaa.
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mambegu Alatuvika Njuli na Patrick Msigwa wamesema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni wazazi kuwa mbali na watoto wao hali inayosababisha wakose malezi bora.
Katika ibada hiyo,Mjumbe huyo wa mkutano mkuu wa wazazi taifa mkoani Njombe Belshaza Mhanga ametoa mpira mmoja kwa timu ya wanawake,sare katika kwaya kuu na ameahidi kutoa mpira wa miguu kwa timu ya wanaume kijijini hapo.
0 Comments