Header Ads Widget

KUNENGE ASEMA WAASISI WA MUUNGANO HAWAKUWA WABINAFSI

 



 MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amepongeza waasisi wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ambapo hawakuwa na ubinafsi wakati wa uongozi wao.


Kunenge aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua Kongamano la miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Mjini Kibaha.


Alisema kuwa viongozi hao Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Amani Karume walikuwa hawana ubinafsi bali walichokuwa wakikitaka ni kuhakikisha wananchi wao wanapata maendeleo.


"Waasisi wetu wote wametuachia matunda mazuri ambayo tunayafaidi ambapo nchi nyingi duniani zimejaribu kuungana lakini zimeshindwa ambapo huu wa kwetu ni wa kihistoria na ni jambo la kujivunia,"alisema Kunenge.


Kwa upande wake Mjumbe wa NEC ya CCM ambaye ni Katibu wa Siasa Uhusiano wa Kimataifa  Kanali mstaafu Ngemela Lubinga alisema kuwa kuna tatizo kubwa la ufundishaji wa somo uraia la watu kujitambua.


Lubinga alisema kuwa bila mshikamano na ushirikiano huwezi kujenga uchumi au jamii bora bila hayo haitapatikana na warendaji wa serikali wanapaswa kuwajibika kutokana na nafasi zao ili kuwatumikia wananchi.


Naye Mwentekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao alisema kuwa Muungano una mafunzo makubwa ambapo Mwalimu Nyerere alihangaika kuunganisha nchi mbali ya Tanganyika na Zanzibar pamoja na za Afrika.


Mlao alisema kuwa anashangaa baadhi ya watu wachache wenye tamaa wanafikiri waasisi hao walikosea kumbe hawakukosea walikuwa na malengo mazuri kuunganisha nchi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI