Halmashauri ya Malinyi imepokea kiasi cha shilingi Bilioni 1.236 kwa ajili ya uboreshaji wa elimu ya msingi kutoka Serikali kuu ambazo zinatarajia kujenga shule mbili mpya na kuongeza madarasa katika shule za msingi na ujenzi wa vyoo.
Fedha hizo zilizotolewa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzan Dk. Samia Suluhu Hassan kwa halmashauri mbalimbali nchini zina malengo ya kuboresha shule za msingi(BOOST) kuanzia ngazi ya awali na miundombinu nyingine kama vyoo na makazi ya walimu.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Malinyi Gaston Silayo amesema fedha hizo zinatarajia kujenga shule mbili mpya moja ikiwa ya mikondo miwili na nyingine ya mkondo mmoja.
Amezitaja shule mpya ambazo zitajengwa kupitia fedha hizo ni Shule ye msingi Mwembeni ambayo itajengwa kwa mikondo miwili na shule ya msingi Manda juu itakayokuwa na mkondo mmoja.
Akifafanua zaidi amesema jumla ya shule nane zimenufaika na mradi huo ambazo ni Mwembeni,Manda juu,Igawa,Kiswago,Madibira,Madabadaba,Njiwa na Mtimbira.
Ujenzi wa shule mbili mpya za Mwembeni mikondo miwili na Manda juu mkondo mmoja zinatarajia kutumia kiasi cha shilingi milioni 782.2.
Aidha katika ujenzi wa shule mpya Mwembeni matarajio ni ujenzi wa madara mawili ya mfano ya awali na matundu yake ya vyoo,madarasa 14 na matundu 18 ya vyoo ambayo kati ya hayo mawili ni ya walimu na 16 ya wanafunzi jingo la utawala pamoja na kichomea taka.
Katika shule ya msingi Manda juu kutakakojengwa shule ya mkondo mmoja yatajengwa madarasa mawili ya mfano ya awali na matundu sita ya vyoo,madarasa saba na matundu 10 ya vyoo ambapo kati ya hayo mawili ya walimu na wanafunzi nane jingo la utawala na kichomea taka.
Bwana Silayo amesema shule sita kati ya nane zinatakazonufaika na mradi wa BOOST zinatarajia kila moja kujenga madarasa mawili kila shule ambayo kwa jumla yote yatakuwa nane yakiwemo yale ya awali ambapo zinatarajia kutumia kiasi cha shilingi milioni 264.
Aidha katika mradi huo pia itajengwa nyumba ya moja ya mwalimu ambayo inatarajia kutumia shilingi milioni 95.
Kaimu Mkurugenzi amesema fedha hizo zitapelekwa moja kwa moja katika shule husika kwa ajili ya kuanza miradi hiyo ya ujenzi na uboreshaji wa elimu ya msingi na awali.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-H/W MALINYI
0 Comments