Header Ads Widget

MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO KUWASILI MKOANI MWANZA KESHO KWA ZIARA YA SIKU MBILI,

 


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Khigoma Malima amesema, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:Philip Mpango anatarajiwa kuwasili katika Kijiji cha Hungumalwa Wilayani Misungwi na mara baada ya kumpokea Makamu wa Rais ataelekea kwenye mradi wa Uzalishaji wa ng'ombe bora wa maziwa na nyama kwenye shamba la Mifugo la Mabuki lililopo Wilayani Misungwi.

Ata hivyo Malima amewakaribisha wananchi wote wa mikoa ya jirani kuja kumpokea kwa shangwe kesho asubuhi akitokea Mkoani Shinyanga.

Amesema lengo la Mkoa wa Mwanza ni kuwahamasisha wananchi kuwa wafugaji bora na mifugo yao iwe na tija kwa maziwa na nyama,pia itakuwa faida kwenye viwanda vya nyama kwa kupata ngo'mbe bora.

"Hapo kwenye mradi wa Uzalishaji wa ng'ombe bora wa maziwa na nyama napenda kuwaona wananchi wengi kwani kuna mengi na muhimu ya kujifunza namna ya ufugaji wa kisasa na siyo uchungaji,kuchunga ni kutembe na ng'ombe umbali mrefu bila ya kuwa na tija yoyote".Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

"Namshukuru Mhe.Rais kwa kutuletea ng'ombe bora 500 ambao wataleta matokeo chanya ya kupata ng'ombe bora,vilevile wapo Vijana 85 wanaoendelea kupata utaalamu wa ufugaji bora hapo Mabuki".Mkuu wa Mkoa.

"Sisi kama Wizara kwanza tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa Mhe.Malima kwa kutambua umuhimu wa shamba hilo la mifugo na kuliingiza kwenye ratiba ya Makamu wa Rais,mpango wetu ni kulifanya shamba hilo kuwa la mfano ukandaa huu wa Afrika Mashariki".Mhe.Abdallah Ulega Waziri wa Uvuvi na Mifugo.

Makama wa Rais Mhe.Philip Mpango siku ya Jumatano saa mbili asubuhi atafungua kikao cha tathmini ya utendaji wa shughuli za Mahakama Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano Malaika Beach Resort,baada ya hapo atapata wasaa wa kuwasalimia wananchi eneo la Buswelu Centre Wilayani Ilemela.

Aidha Malima amesema kuwa, Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt Mpango akiwa njiani kuelekea kurudi Dodoma  atasimama eneo la Kisesa Wilayani Magu na kuwasalimia wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI