Header Ads Widget

JAMII MKOANI LINDI YATAKIWA KUKEMEA MMOMONYOKO WA MAADILI





Na HADIJA OMARY MATUKIO DAIMAAPP,LINDI

.MKUU  wa Mkoa wa Lindi   Bi. Zainab Telack ameitaka jamii mkoani humo kukemea  vitendo viovu vinavyokiuka misingi ya Maadili  ikiwemo matendo ya ulawiti na badala yake waishi kwa kuzingatia Mila na desturi ya kitanzania.

 Telak  ametoa wito huo jana  wakati wa mkutano wa wadau wa elimu ulioenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa elimu 2023 na sherehe za utoaji wa tuzo za ufaulu wa mitihani na pimaji za mwaka 2022/2023  uliofanyika katika viwanja vya Ilulu Manispaa ya Lindi mkoani humo .


mkutano huo uliobeba kauli mbiu inayosema Uwajibikaji wangu ni msingi wa kuinua ubora wa elimu na ufaulu mkoa wa Lindi .


Telack alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kutambua suala la malezi ya mtoto ni mtambuka na kwamba halimuhusu mzazi pekee bali ni la jamii mzima.




Alisema maendeleo ya wanafunzi  kitaaluma yanategemea sana uwepo wa walimu shuleni yapo mambo ambayo yanaendelea kwa Watoto nje ya wazazi wao hivyo wanapaswa kuyaangalia.



“ukishakuwa mwalimu hata uwe na miaka 13 tayari wewe ni mzazi, na wazazi wanawakabidhi watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni tunaomba muwaangalie sana kwa sababu hawa Watoto ni wadogo zenu na pia ni Watoto wenu tunaomba muwe na uchungu nao”



Awali akitoa salamu za chama cha mapinduzi CCM katibu wa chama hiko Wilaya ya Lindi Asha Mwendwa Aliwaomba waalimu kuendelea kukemea matendo maovu ambayo sasa yanafanyika na  kuonekana kwenye mitandao mingi  ya kijamii.



“Wakati mwingine tunawakabidhi Watoto mnashinda nao shuleni na mnalala nao shuleni naomba kama mzazi kama mama tuendelee kuyakemea yale yanayoendea kufanyika kwenye mitandao ya kijamii” mwendwa 

 

Aliongeza kuwa endapo vitendo hivi vinavyoendelea visipokemewa na kukomeshwa basi hata dhamira ya Rais Samia ya kutoa fedha kwa ajili ya kutengeneza miundombinu mashuleni haitafikiwa kwani baada ya miaka kumi hijayo hakutakuwa na wototo wa kusoma kwani kizazi chote kitakuwa kimehalibika.

Nae Mwalimu Mkuu shule ya msingi Great Mindi iliyopo mtaa wa  Mingoyo Manispaa ya Lindi,  Magreth Nnko alisema ili kuzuia na kuwakinga wanafunzi na matendo hayo shule yao wameweka utaratibu wa kuzungumza na Watoto juu ya kujilinda na maswala ya ulawiti wakati wa kufunga na kufungua shule.

“ tunazungumza nao hasa kwa kuzungumza nao lakini hasa kuwapa haka ka kauli mbiu ambako kanakataza kuwagusa kwenye maeneo yao ya siri mfano kwenye matiti ama kwenye tupu zao” alieleza Nnko 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI