NA HADIJA OMARY LINDI.....
Viongozi wa vyama vya ushirika wa Wilaya za Ruangwa Nachingwea na Liwale vinavyohudumiwa na chama kikuu cha ushirika ( RUNALI) wametakiwa kujiimarisha kiuchumi na kuachana na mtindo wa kutegemea wahisani kwa mikopo yenye riba kubwa hatua inayofifisha uwezo wa kuhudumia wanachama
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma alipokuwa akifunga mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi yaliyofanyika katika ghara la Runali Wilayani Ruangwa.
Ngoma alitumia fursa hiyo kuwasisitiza viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika kuvifanya vyama vyao kuwa imara kwa kuwa na miradi ya maendeleo na kuongeza wanachama kwani ushirika ni biashara .
DC Ngoma pia alisema ni imani yake mafunzo hayo yatawasaidia viongozi wa ushirika kufanya mabadiliko na kukuza ufanisi na kuwa chachu ya maendeleo kwani yamefundisha mambo mengi ikiwemo namna ya kuandaa bajeti,kutunza vitabu vya fedha , kumbukumbu na nyaraka.
"vyama ni tasisi lazima vikuze ufanisi kwa wanachama na kuwa na miradi ya maendeleo na kusaidia jamii yenye uhitaji"amesema Ngoma.
Kwa upande wake Meneja mkuu wa chama kikuu cha ushirika RUNALI Jahida Hasani amesema chama kimeendesha mafunzo hayo kwa viongozi vyama vya msingi lengo kubwa ni kuwejengea uwezo, kwenye nyanja mbalimbali kama uandikaji mipango biashara utunzaji kumbukumbu uandishi wa vitabu vya fedha ili waweze kuondoa tatizo la upatikanaji wa hati chafu.
"Mafunzo haya ni mwendelezo kwani chama kinafanya zoezi kama hilo kila mwaka ili kuwajenga viongozi wake" amesema Jahida
Nae Mkaguzi kutoka COASCO Hansi Kishiwa aliwasisitiza viongozi hao wa vyama vya ushirika kutunza taarifa katika nyaraka ili kupunguza migogoro katika ushirika vyama vyao
" Kupitia elimu niliyoitoa ni imani yangu itawasaidaia kwani baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika imekua changamoto kuweka hali halisi ya thamani ya mali za vya ushirika katika taarifa zao lakini pia utunzaji wa nyaraka za ushirika pia imekua ni changamoto ambayo inasababisha bodi zinazochaguliwa kushindwa kujua taarifa za bodi iliyopita hivyo" alisisitiza Kishiwa
0 Comments