Header Ads Widget

BARABARA YA KIBOSHO SHINE-KWA RAPHAEL-INTERNATIONAL SCHOOL KWENDA KUKAMILIKA KWA KIWANGO CHA LAMI.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ipo katika mpango ya kutafuta fedha ili kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kibosho shine-Kwa Raphael hadi International school kwa kiwango cha lami Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.


Hatua hiyo imekuja mara baada ya Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Patrick Ndakidemi kuipambania barabara hiyo ambapo jana alihoji Bungeni ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kipande kidogo kilichobakia kukamilika kwa kiwango cha lami.


Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alisema kuwa, Serikali inatambua kazi kubwa imeshafanyika hivyo inaendelea kutafuta fedha ili kumalizia kipande hicho kilichobakia na wananchi waweze kupata huduma iliyolengwa na Serikali.


Hatua hiyo imeleta faraja na matumaini makubwa kwa wananchi wa Kibosho kwani barabara hiyo ndio mkombozi wa maendeleo yao.


Anne Lyimo alisema kuwa, kipande hicho cha barabara kilichokuwa kimebakia kujengwa kitakapokamilika kitasaidia kufungua maendeleo kwani kipindi cha mvua barabara hiyo ilikuwa ikipitika kwa tabu sana na kupelekea kupata changamoto ya kufikisha mazao yao sokoni.


Anne alitumia pia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Prof Patrick Ndakidemi kwa jinsi ambavyo amekuwa akipambana kuhakikisha anatatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.


"Ni miaka mitatu sasa tangu tumpe ubunge Prof. Ndakidemi lakini ametuonyesha kwa vitendo nia yake ya kuwatetea wananchi na kuwaletea maendeleo tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu ili uendelee kutupigania sisi wananchi wako tuliokupa hiyo dhamana" alisema Anne.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI