Header Ads Widget

WAVUVI WADOGO BAGAMOYO WASHAURI KUCHANGAMKIA FURSA YA MIKOPO



Mwandishi wetu


Mkurugenzi wa Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development Bwana Edwin Soko amewashauri wavuvi wadogo wa bandari ya Bagamoyo kuchangamkia fursa za mikopo ili wafanye uvuvi wenye tija.


Soko ameongea hayo kwenye ziara  iliyomkutanisha na wavuvi wadogo kwenye bandari ya bagamoyo, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambao wanavua kwenye Habari ya Hindi.


Baadhi ya wavuvi walitoa changamoto zao za kukosa mitaji  na  kujikomboa kwa kufanya uvuvi mkubwa .


Bwana Hassan Juma ambaye ni mvuvi alisema kuwa kinachomkwamisha ni kukosa mtaji wa kuwa na boti yake ya uvuvi na hivyo kuishia kuajiriwa kila Mwaka.



Pia Bwana Kombo Juma alibainisha kuwa, amekosa mtaji wa kununua nyavu ili aweke kwenye mtumbwi wake na hivyo kulazimika kuajiriwa kwa mtu mwingine.


Kufuatia kuibuliwa kwa changamoto hizo Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko aliwashauri wavuvi wadogo kutoogopa kukopa ili kupata mitaji ya kununua baadhi ya zana za uvuvi kwani mahitaji ya mazao ya uvuvi ni makubwa hivyo wasiopgope kukopa.



Soko aliongeza kuwa TMFD ina  sera za ustawi wa wavuvi wadogo kiuchumi hivyo ina wajibu wa kumulika changamoto za wavuvi kiuchumi.




Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko ameipongeza serikali kwa kujenga soko la samaki la BAGAMOYO alipotembelea soko hilo lililoko wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwana na kuona namna soko hilo lilivyo na mchango mkubwa kwenye sekta ya uchumi.


Soko amesema Serikali imefanya jambo sahihi kwani kutokana na Bagamoyo kutegemea sana shughuli za uvuvi kuwa na soko la kisasa limeongeza kasi katika uchumi 


Pia Soko ameongeza kuwa soko hilo la samaki linaongeza aina ya vivutio vya utalii Bagamoyo kwa kuwa watalii wengi kwa sasa wanatembelea soko hilo na kujionea aina tofauti ya samaki wanaouzwa sokoni hapo.


Pia ametoa rai kwa wavuvi wadogo kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani kwenye kutunza kuzuia upotevu wa mazao ya uvuvi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI