Header Ads Widget

WANAFUNZI WASICHANA WANAOSOMA SAYANSI WAELEZA VIKWAZO VINAVYOWAKUMBA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


WANAFUNZI wasichana wanaosoma masomo ya sayansi wameiomba serikali kuwawekea mazingira mazuri ambayo yatawafanya ndoto zao za kusoma masomo hayo zitimie na kuwa na ufaulu wa juu.


Wanafunzi hao walisema hayo katika kongamano la wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa ya Kigoma,Tabora na Songwe kujadili changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo ili kufanikisha malengo yao.



Mwanafunzi huyo alisema kuwa wanafunzi wengi wa kike wana hamu ya kusoma masom ya sayansi lakini hata shuleni na nyumbani  kuna maneno ya kukatisha tama wanafunzi kwamba masomo hayo nit a wavulana hivyo wasichana wakisoma hawatafanya vizuri.


Kwa upande wake Mwanafunzi Aneth Lucas kutoka wilaya ya Urambo mkoani Tabora alisema kuwa ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi ni changamoto kubwa inayofanya wanafunzi wengi hasa wasichana kukimbia masomo ya sayansi hata kama wanayapenda.



Mwanafunzi mwenye ulemavu wa kusikia kutoka shule ya sekondari Kazima mkoa Tabora,Evodia kimath alisema kuwa wanafunzi wenye ulemavu wana changamoto kubwa katika kusoma masomo ya sayansi kutokana na miundo mbinu duni ya kujifunza na kufundishia iliyopo hali inayokatisha tamaa wengi wao kuacha kusoma masomo hayo hasa Kemia,Fizikia na Baiolojia.


Kwa upande wake Mwakilishi wa wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa,Dk.Yangson Mgogo ambaye ndiye Mratibu wa mpango wa kuinua kiwango cha wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya sayansi unaotekelezwa kwa pamoja baina ya serikali na Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) alisema kuwa wameanza kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wanafunzi wasichana wanaosoma masomo ya sayansi.


Akizungumza wakati akifunga kongamano hilo Waziri wa nchi ofisi ya Raisi TAMISEMI,Angellah Kairuki alisema kuwa serikali imeanza kutekeleza mpango wa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kuanzia shule za sekondari hadi vyuo vikuu.



Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Shukuru Kalegamye alisema kuwa wanatambua changamoto hiyo hasa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na kubainisha kwamba hali ilivyo sasa ni tofauti na huko nyuma.


Alisema kuwa mwaka 2020 wanafunzi wa kike 120,000 walikuwa wamesajiliwa kusoma masomo ya serikali na kwamba kufikia mwaka 2022 idadi hiyo ilipanda na kufikia 124,247 na idadi itaongezwa maradufu na taratibu nzuri za kuwafanya wanafunzi hao wafikie malengo yao zinazidi kuboreshwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI