Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
Kutokana na utafiti uliofanywa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi kuhusu usajili wa sehemu za kazi pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini ilibainika uwepo wa ada ambazo zilikuwa zinaongeza gharama za uendeshaji na kuchangia sehemu nyingi za kazi kutokidhi matakwa ya Sheria na kufifisha ushindani wao kibiashara.
OSHA ilipendekeza ada hizo kupunguzwa ama kufutwa ambapo Mhe. Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia ada hizo kufanyiwa marekebisho kwa kuondoa na kupunguza jumla ya Ada / Tozo kumi na tatu 13.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi Khadija Mwenda Amebainisha hayo Jijini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokua akieleza utekelezaji wa majukumu ya Wakala pamoja na mafanikio Yaliyopatikana katika uongozi wa serikali ya awamu ya Sita.
“Ada zilizoolewa ni pamoja na Ada ya Usajili wa eneo la kazi iliyokuwa ikitozwa kati ya Sh. 50,000 hadi Sh.1, 800,000, Ada ya fomu ya usajili sehemu za kazi iliyokuwa ikitozwa Sh. 2,000,Kufuta Faini zinazohusiana na ukosefu wa vifaa vya kuzimia moto ya Sh. 500,000, Kuondoa Ada ya Leseni ya Ithibati iliyokuwa inatozwa Sh 200,000 kwa mwaka, Ada ya Ushauri wa kitaalamu wa Usalama na Afya ya Sh 450,000”.Alisema Bi. Mwenda
Mwenda Ameendelea kusema Ada zingine Zilizofutwa kuwa ni Ada ya mafunzo ya elimu kwa umma iliyokuwa inatozwa kiasi cha Sh. 250,000 kwa kila mshiriki, Kupunguza ada ya uchunguzi wa ajali iliyokuwa ikitozwa Sh. 500,000 mpaka Sh. 120,000, Kuondoa ada ya Kipimo cha Mzio (Allergy test) iliyokuwa ikitozwa Sh. 25,000 kwa Mfanyakazi.
“Ndugu zangu Ada ya Kipimo cha Kilele cha Upumuaji (Peek Expiratory Flow test) iliyokuwa ikitozwa Sh. 10,000 kwa Mfanyakazi imefutwa , Tumepunguza ada ya huduma za ukaguzi wa mifumo ya umeme katika Vituo vya Mafuta vilivyopo vijijini kutoka Sh. 650,000 hadi Sh. 150,000. Punguzo hili lililenga kuhamasisha uwekezaji katika maeneo hayo, hivyo kupunguza athari zinazoweza kutokea kutokana na utunzaji wa mafuta kwenye chupa za maji na madumu, suala ambalo linahatarisha maisha ya wananchi katika maeneo hayo”Alisema
0 Comments