Header Ads Widget

PROFESA PATRICK NDAKIDEMI "SERIKALI IMETOA BILIONI 1.9 KWA AJILI YA MAENDELEO KATA YA KIBOSHO KINDI"

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani imetoa fedha zaidi ya Bilioni 1.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika kata ya Kibosho Kindi wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.


Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi alipofanya ziara katika kata hiyo na kufanya mkutano na wananchi uliofanyika viwanja vya KNCU Kindi kati kueleza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha miaka miwili.



 Prof. Ndakidemi alisema kuwa kwa kipindi hicho kifupi, Serikali imetekeleza  miradi mbali mbali katika sekta ya afya, elimu, barabara, maji na maendeleo ya jamii yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.9. 

Alisema kuwa vipo pia vikundi vilivyonufaika na mikopo ya Halmashauri ni vingi na wanaendelea kuomba.

Wananchi waliohudhuria katika mkutano huo walieleza kero swala la Kindi SACCOS ambapo fedha za wanachama hazijulikani ziko wapi. 



Kero nyingine ni suala la lami iliyokuwepo Kindi kuuzwa bila utaratibu wa kueleweka hali inayoleta sintofahamu kwa wananchi na kumuomba Mbunge huyo kufwatilia fedha iliyopatikana baada ya kuuzwa lami hiyo.


"Ipo kero ya bima ya afya kwa wazee kwani wanapata adha kubwa pindi wanapokwenda kupata matibabu pamoja na suala la shamba la Kindi Kale kuwa na migogoro, na mapato hayajulikani yanakwenda wapi" walisema Wananchi.



Akijibu kero hizo, Prof. Ndakidemi aliahidi kufikisha swala la lami kwa uongozi wa Wilaya. 

Alisema kuwa swala la Kindi SACCOS lilikuwa linashughulikiwa na mkuu wa wilaya, na kuwasihi wawe na subira kwani jibu litapatikana na kuhusu bima ya afya kwa wazee, Mbunge amewambia wazee wawe na subira kwani swala hilo linafanyiwa kazi na wanategemea bunge litapitisha sheria ya bima ya afya kwa wote muda mfupi ujao.



Aidha Mbunge huyo aliwaomba wananchi wamuunge mkono Rais, Mbunge na Diwani kwenye harakati zote za kuwaletea maendeleo.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI