Header Ads Widget

YANGA SC YAWEKA BAYANA MATAYARISHO YAO KUELEKEA MCHEZO WAO WA SHIRIKISHO KESHO DHIDI YA REAL BAMAKO

 



Na.Dickson Bisare Matukio Daima TV Dare salaam.



KOCHA mkuu wa timu ya Yanga Sc Nasdine  Nabi ameongea kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Real Bamako timu kutoka Mali kombe la Shirikisho Barani Afrika mchezo utakaopigwa kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium jijini Dar es salaam.



Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amesema yeye anafahamu mchezo wa kesho utakuwa siyo mchezo rahisi kwani katika mchezo wake dhidi ya Tp Mazembe walipata ushindi na wanaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa kuelekea mchezo huo.



"Natambua mchezo wa kesho utakuwa ni mchezo mgumu lakini naamini kwa yote niliyowaelekeza wachezaji wangu naamini katika nchezo wa kesho tutafanya vyovyote vile tuweze kupata matokeo chanya." Amesema Nasdine Nabii Kocha Mkuu wa Yanga Sc. 



Sambamba na hilo Kocha Nasdine Nabii Kocha wa timu ya Yanga Sc kwa mujibu swali kutoka kwa wanahabari ametoa ufanunuzi kuelekea wachezaji ambao ataenda kuwakosa katika mchezo wa kesho kwa kubaini kwamba mchezaji ambaye atakosa ni Abbakary Salum (Sure Boy) ambaye ameondokewa na mtoto wake leo Asubuhi (Amefiwa).



Lakini pia kocha ameenda mbele na kutaja mchezaji mwingine ambaye huenda akakosekana kwenye mchezo wa kesho ambaye ni Jesus Moloko ambaye alipata majeraha kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Real Bamako ya nchini Mali.




Naye, Mwaakilishi wa wachezaji wa Timu ya Yanga Sc Bacca amesema wao kama wachezaji wana uchungu na mchezo wa kesho na wanatambua matokeo walioyapata kwenye mchezo wao dhidi ya Rea Bamako hayakuwa ya kuridhisha na wanatambua kwamba wana deni kwa mashabiki wao wanaowafuatalia.



"Sisi kama wachezaji wa timu ya Yanga Sc tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho na tunaenda kwenye mchezo huo tukiwa tunafahamu kwamba wapinzani wetu Real Bamako wamekuja kucheza mpira na hawajaja kutalii,hivyo basi,sisi kama wachezaji tutahakikisha kila tuwezalo kwenye mchezo wa kesho tumepata matokeo chanya na kurudisha furaha kwenye klabu lakini pia kuwapa furaha mashabiki wetu."Amesema Bacca Mwaakilishi wa wachezaji Yanga Sc.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI