Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika lisilo la kiserikali la WWF linalojishughulisha na masuala ya misitu wa Hifadhi ya Mazingira duniani tawi la nchini Tanzania Dr. Amani Ngusaru amewataka Watanzania kupanda miti kwa wingi kama hatuna akili nzuri ili kulinusulu taifa na vimbunga na mafuliko ya mara kwa mara kama yanayotokea nchini Msumbuji.
Amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es salaam wakati akizungumzia Kampeni ya dakika 60 ya kila Mtanzania kuzungumzia au kufanya jambo linalohusu utunzaji wa mazingira duniani.
Alisema kila mtanzania achukue taadhali kwa nchini yetu kupata athari za uharibifu wa mazingira kwa kupanda miti kwa wingi kwakuwa vimbunga na mafuliko ni matukio yasiyotabirika duniani.
"Ili kama tunasema kubadilisha mifumo ya Mvua kwa Njia ya kupanda miti basi tuongeze kiasi chetu Cha upandaji miti na kuitunza ili tubadili kabisa hali ya tabia nchi tupate mvua za uhakika hata mkulima alime kwakutegemea kupata mvua za uhakika katika Majira Sahihi" alisema Dr. Ngusaru.
Alisema serikali imejidhatiti na inatejeleza mpango huo wa kuthibiti athari za uharibifu wa mazingira nchini ambapo viongozi wote wa juu wa serikali mara kwa mara huzungumzia hamasa ya upandaji miti lakini Wananchi kwa mbalimbali wamekuwa na mwitikio mdogo katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira.
0 Comments