Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wafanyakazi wa sekta za umma na binafsi mkoani Njombe wamelalamikia hujuma zinazofanywa na waajiri wao katika kuchagua wafanyakazi bora wakati wa sherehe za mei mosi pamoja na kushindwa kuwapa zawadi kadri wanavyowaahidi
Katika kikao kilichowakutanisha baadhi ya viongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi na mkuu wa mkoa wa Njombe baadhi ya wafanyakazi hao akiwemo Luchabiko Kitalinga,Calvin Mtewele,Mwalimu Varian Ngalioma na Festo Mbakilwa wamesema kumekuwa na hujuma nyingi katika kuwapata wafanyakazi bora huku taasisi binafsi zikiwa na ubabaishaji mwingi kwa wafanyakazi wao.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema atakutana na waajiri wote mkoani Njombe ili kujadili malalamiko ya wafanyakazi hao na kwamba hakuna wajibu bila haki.
Aidha Mtaka amewataka waajiri hao kuacha kupandisha mabega kwani mabaya na mazuri hulipwa hapa hapa duniani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA mkoa wa Njombe Dokta Mashaka Kisulila amesema wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali dhidi ya waajiri wababaishaji ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya kuwatimizia wafanyakazi stahiki zao.
Kutokana na makabidhiano ya Mwenge kati ya mkoa wa Njombe na Iringa hapo Mei Mosi mwaka huu,Shughuli nyingi za mei mosi zitafanyika aprili 30 mwaka huu Katika mkoa wa Njombe ili kupunguza majukumu ya siku ya tarehe 1 mei.
0 Comments