Header Ads Widget

ACT WAZALENDO YAITAKA SERIKALI KUPITIA MFUMO WA TAASISI ZA MIKOPO NCHINI

 


Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga. 


Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kupitia upya mfumo mzima wa ukopeshaji toka Taasisi zisizo za Kiserikali zinazotoa mikopo na kuangalia riba zao kutokana na kuwa  mzigo kwa wanawake na kupelekea kushindwa kurejesha na kukimbia familia zao


Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara Dorothy Samu wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa ACT lililofanyika Jijini Tanga ambapo alisema mikopo hiyo badala ya kuwa mkombozi kwa wanawake imekuwa mizigo kwao.


Dorothy alisema kuna ulazima kwa Serikali iangalie kwa umakini riba ambazo zimetolewa na taasisi hizo ambazo sio himilivu na sio rafiki kwa wanawake ambao ndio wakopaji wakubwa katika kuendeleza biashara zao za ujasiriamali.


“Serikali inapaswa kuangalia kwa makini taasisi hizi za mikopo ambazo zimekuwa na riba kubwa,sisi wanawake ndio tunaokopa na ndio tunaoadhirika tunaposhindwa kupeleka marejesho na ndio maana wanawake wengi wanayakimbia makazi yao  “Alisema.


Alisema Serikali iweke utaratibu mzuri katika mikopo inayotolewa na Halmashauri kupitia pato la ndani na kuacha kufanya ubaguzi wa utolewaji wa mikopo hiyo kutokana na itikadi za vyama jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa Taifa. 



Aidha alisema ngome ya wanawake ACT inalengo la kuwasemea wanawake wa Tanzania ili Serikali itengeneze Sera nzuri za kumkomboa mwanamke ambae ndio nguzo ya maendeleo ya Taifa na  familia kwa ujumla.


Awali akizungumza Waziri Kivuli wa Wizara ya Wanawake,Watoto na Makundi Maalumu Janeth Rite aliitaka Serikali kuhakikisha Halamshaueri zinakuwa na uwiono sawa katika utoaji wa fedha za mikopo asilimia 10 zinazotokana na mapato ya ndani.


Alisema haki ya wanawake itolewe kwa wanawake wote Nchi nzima na kuacha vitendo vya ubaguzi na kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu zilizopangwa na Serikali juu yabutolewaji wa asilimia 10 kwa makundi maalumu.


“Suala hilo la mikopo zinazotoka kwenye Halmashauri lazima kuwepo na usawa pamoja na kuondosha upendeleo ambao umekuwa ukipelekea manunguniko kwa wanawake kutokana na itikadi zao za kiasiasa”Alisema


Rite alisema wanawake ndio wanaobeba majukumu ya kifamilia na ndio waliosahaulika katika mifumo bora ya kuwezeshwa ili waweze kujiinua katika shuguli za ujasiriamali.


Aidha alisema kwamba kwa mujibu wa takwimu zilizopo ni asilimia 80 ya wanawake wapo kwenye  sekta ya kilimo ambao wanalima kwa kutumia jembe la mkono kilimo ambacho hakina tija kwao kutokana na kupata mazao hafifu.



Alisema kwa sababu hakina tija ndio maana Chama hicho katika mipango yao watakapo pata ridhaa ya kuongoza nchi watawaondoa kwenye ujasiriamali usiokuwa na tija ikiwemo kuwapeleka wenye tija ambao wanaweza kukopesheka.


Hata hivyo aliwakumbusha wakina mama kuwa mfumo wanaotumia wa kilimo cha mkono wakiendelea nao  wasahau mafanikio kupitia sekta hiyo ya kilimo na ipo haja ya kubadilika ili wawe wakulima wa kilimo cha kisasa na change tija.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI