Header Ads Widget

TPDC YAPONGEZWA KWA UTENDAJI MZURI WA KAZI

 



Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Japhet Hasunga amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC) kwakusimamia vema miradi ya gesi asilia nchini ambayo Kwa Sasa inachangia Zaidi ya asilimia 60 ya uzalishaji wa umeme nchini.


Kauli ameitoa wakati walipotembelea miradi hiyo ya Madimba na Mnazibay Mtwara ambapo visima zaidi ya vitano vinavyofanyakazi vyote ambapo miradi mbalimbali inaendeshwa na gesi hiyo sambamba na matumizi ya majumbani. 


“Ipo miradi mikubwa ya Gesi asilia nchini ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika Maendeleo ya nchi ikiwemo matumizi ya gesi majumbani, viwandani na kwenye magari hali ambayo imekuwa ikichagiza maendeleo kwa kiasi kikubwa mfano matumizi ya Gesi majumbani, vyuoni kwenye magari viwandani ni hatua kubwa Kwa nchi" alisema Hasunga


Ziara yetu ina Lengo la kuangalia Fedha  zimetumikaje katika miradi ya gesi asilia licha ya uwepo wa mradi wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar  kuzalishia umeme lakini tumeridhishwa na miradi hii ni jambo la kufurahisha kuona watu wa Lindi na Mtwara wakitumia gesi asilia majumbani" alisema Hasunga 


Nae Esther Matiko Mbunge na Mjumbe wa Kamati PAC alisema kuwa nchi imekuwa na matumizi ya Kuni na mikaa Hali ambayo imekuwa ikipelekea uharibifu wa mazingira hivyo uwepo wa gesi utaokoa mazingira Kwa kiasi kikubwa. 


"Mazingira yamekuwa yakiharibiwa kwa kiasi kikubwa na ukataji wa miti hovyo kwaajili ya kuni na kuchoma mkaa kitendo cha vyuo na shule kutumia pia gesi  asilia kwaajili ya kupika kinaweza kusaidia jamii kwa kiasi kikubwa na kupunguza uharibifu wa mazingira"


Mjumbe wa Bodi ya TPDC Dismas Fuko  alisema kuwa ujio wa Kamati hiyo kuona miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji ambao tunaamini kuwa tunafanikiwa katika utekelezaji. 


"Tumefanikiwa kiasi kikubwa katika miradi hii ambapo ni asilimia 60 ya umeme unaotumika nchini huzalishwa kwakutumia gesi asilia ambayo Kwa Sasa inatumika majumbani, vyuoni, viwandani na kwenye magari" alisema Fuko




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI