Header Ads Widget

TARI YAWAPONGEZA WAKULIMA WA UFUTA MANDAWA

 


Mtwara, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI Naliendele Kitengo cha Program ya Ufuta kimewapongeza wakulima wa kijiji cha Mandawa Wilayani Kilwa kwakuwa na shamba darasa zuri linaloweza kuwavutia wakulima kujifunza na kulima zaidi zao hilo hivyo kuwapa mbolea ya maji na dawa ya viadudu visumbufu katika zao hilo.


Mratibu wa Program ya zao la Ufuta Kitaifa Joseph Nzunda amesema kuwa shamba hilo ni mfano mzuri kwa wakulima kujifunza zaidi.


“Tulileta mbegu aina mbili lakini kwa maeneo haya tunaona mbegu aina ya mtondo2013 imefanya vizuri pia wamehudumia shamba vizuri tumevutiwa na kikundi hiki cha jipemoyo kata ya mandawa na kijiji cha madawa ambapo shamba hili liko barabarani ambapo wakulima wengi wanapita na kujifunza zaidi tutaendelea kuleta kulingana na mahitaji ya wakulima”


“Wameonyesha moyo ingawa kuna changamoto ya vijidudu ndio maana tumeona tuwawezeshe na kuwaletea zawadi kidogo kwaajili ya kuboresha shamba ili tusipoteze mbegu hii muhimu kwa wakulima wa eneo hili” alisema Nzunda



Nae Ofisa Kilimo msaidizi kutoka TARI Naliendele Nicko Lukoya alisema kuwa kikundi hicho kimekuwa kikifata maelekezo ya wataalamu na kufanya vizuri.


“Tumetembelea hili shamba kata ya mandawa kata ya kibaoni tunaona shamba wamelima vizuri wamepalilia na kuweka dawa za kudhibti wadudu tunawashauri waendselee kutumia mbolea za maji na dawa za kuua wadudu kwa kuwatia moyo tumewapa mbolea ya maji na dawa ya kuuwa wadudu ili waendelee kufnaya vizuri zaidi”


"Shamba hili litataoa somo kubwa kwakuwa ni dogo na lio njiiani tunaamini kupitia hapa tunaweza kushawishi wakulima kubadilka na kuchukua tekenolojia hii na kuipeleka katika mashamba yao"


Nae Rabia Amanzi mkulima wa Kijiji cha Mandawa Wilayani Kilwa alisema kuwa elimu na utaalam waliopewa na Watafiti umekuwa msaada mkubwa kwetu. 


"Watalaamu wamekuwa msaada mkubwa kwetu na wametupa vitendea kazi tunaamini kuwa hiziombegu bora zitatusaidia kutufanya tubadilke na kuanza kulima kisasa zaiid tunaamini kuwa msimu ujao tutafanya vizuri zaidi"alisema 



Halima Hassan mkulima wa Kijiji cha Mandawa alisema kuwa walipata mbegu hizo na kuzipanda kama shamba darasa. 


"Tuliletewa mbegu hizo na tulizipokea na kuanza kuzifanyia kazi kwa kuandaa mashamba na japo ni eneo dogo lakini tulifanikiwa kupanda mbegu aina mbili ambazo ni lindi202 na mtondo 2013 hzi mebgu aina ya mtondo zimekuwa ni mbegu bora katika eneo hili tunawashauri wakulima wasikate tamaa"


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI