Chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) mkoani Iringa, kimetoa msaada wa mashuka kwa wodi ya wanawake katika hospitali teule ya Tosa maganga iliyopo mkoni Iringa.
Katibu wa chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) mkoani Iringa,Uhuru Kitabuka amesema nje ya msaada huo, pia wametoa elimu ya kwa watumishi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSSF na PSSF lengo likiwa ni kuwasaidia wafanyakazi wa hospitali hiyo kufanyakazi katika mazingira mazuri.
Naye katibu wa TUGHE upande wa wanawake Deba Ngwamba, amesema idara ya wanawake mkoa wa Iringa iliona kunauhitaji wakurudisha kwa jamii kile ambacho wamekuwa wakipata katika kazi yao.
Akishukuru kwa niaba ya watumishi wa Hospitali teule ya Tosa
Maganga Dkt Maziku amesema mashuka hayo yatakwenda kuwasaidia wagonjwa kwa kupata mashuka masafi na kwa wakati pamoja na kuikumbusha wadau wengine na jamii kuwa na moyo wa kutoa msaada mbalimbali, katika maeneo ambayo yanauhitaji kwa jamii kama hospital.
0 Comments