Header Ads Widget

SHIRIKA LA TMFD LABAINI BAADHI YA WAVUVI KUTOKUWA NA UJUZI WA KUOGELEA



Mwandishi wetu

Mwanza


Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development (TMFD) limebaini baadhi ya wavuvi kufanya shughuli za uvuvi bila kuwa na utaalamu wa kuogelea jambo linaloongeza hatari kwenye shughuli za uvuvi.


TMFD ilitembelea baadhi ya maeneo ya uvuvi Jijini Mwanza na kubaini wimbi kubwa la wavuvi kufanya shughuli za uvuvi bila kuwa na ujuzi wa kuogelea.



Bwana Robert Charles Mwenyekiti wa Kikundi Shirikishi cha Ulinzi wa Rasilimari za Uvuvi (BMU) kwenye mwalo wa Mswahili Jijini Mwanza amesema kuwa, tatizo hilo ni kubwa kwani wavuvi wengi kwa sasa hawana ujuzi wa kuogelea na wanaingia majini kwa tamaa ya kupata fedha bila kujali usalama wao.


"Unajua kwa kawaida mvuvi lazima ajue kuogelea ili hata kama kuna ajali itatokea aweza kujiokoa kirahisi lakini kama hawana ujuzi huo ni wazi ajali ikitokea maafa yatatokea tu hivyo tunaomba Serikali na wadau kama TMFD watupatie mafunzo ya kuogelea" Alisema Charles.



Naye Bwana Baraka Masunga ambaye ni mvuvi amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wavuvi ambao hawajui kuogelea na kusema hali hiyo ina hatarisha usalama wao kwa kiasi kikubwa..


Naye Mkurugenzi wa Shirika la TMFD bwana Edwin Soko alisema suala la usalama ni muhimu sana hivyo kuna umuhimu mkubwa sasa wa kuandaa mafunzo ya kuwafundisha wavuvi namna ya kuogelea ili kuongeza weledi kwao.



" Tutaandaa mpango mzuri wa kuandaa mafunzo kwa ajili ya wavuvi hii itasaidia kuimarisha usalama wao wawapo majini" Alisema Soko.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI