Teddy Kilanga Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amemaliza mgogoro wafanyakazi na uongozi wa kiwanda cha uchakataji wa Chuma
(Steel Lodhia) uliodumu kwa kipindi cha siku mbili kwa kile kinachodaiwa maslahi madogo ya wafanyakazi na usalama mdogo mahali pakazi hali iliyopelekea mamia ya wafanyakazi hao kugoma kuendelea kufanya kazi.
Mtahengerwa amemaliza mgogoro huo kwa kuwakutanisha uongozi wa kiwanda hicho pamoja na wafanyakazi hao zaidi ya 500 katika kutafuta suluhu ya pande hizo mbili ili kila mmoja aweze kunufaika kulingana na utendaji wa kazi kazi wake.
Mkuu huyo amesisitiza uongozi wa kiwanda hicho kusimamia na kutekeleza haki za wafanyakazi wake pamoja na kuongezewa mishahara inayokidhi mahitaji yao ya kimaisha.
"Hata hivyo amesisitiza wafanyakazi hao kuwa waaminifu mahali pa kazi na kuachana na vitendo vya wizi hali ambayo inapelekea kutoaminiwa kazini,"amesema Mtahengerwa.
Amewataka wafanyakazi hao kuendelea na kazi kwani serikali imekubaliana na menejimenti hiyo katika kuhakikisha maslahi bora ya wafanyakazi yanaboreshwa ikiwemo mishahara na malipo ya ziada ya kazi
"Kunamambo ya kiutumishi tumewekana sawa ikiwemo uwepo wa vifaa vya kazi zinavyokidhi ubora wa kazi na waliotoa hoja za madai mbalimbali wasifukuzwe bali wafanye kazi na kama wakifukuzwa wawe wamefanya makosa mengine na si haya ya haki zao"
Naye Mwenyekiti wa kampuni za Lodhia Group ,Harun Lodhia amesisitiza yaliyotokea yamesawazisha na lengo kubwa wafanyakazi wapate ajira na kuahidi kuongeza fedha kwa wafanyakazi ikiwemo kiwango cha mshahara kwa group zote za wafanyakazi wa kiwanda cha kutoka 150,000 hadi 180,000 na kusisitiza wafanyakazi kufanya kazi pale wanapolipwa mishahara yao.
"Kila mwaka mara mbili watafanya vikao na wafanyakazi hao,naomba tusameheane sisi sote ni binadamu tufanye kazi na mkipata mshahara msilale njooni kazini"
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wameishukuru serikali na kampuni ya Lodhia kwa kuwasikiliza na kuongeza kiwango cha mshahara kwani hapo awali fedha ya mshahara ilikuwa haikidhi mahitaji yao muhimu.
0 Comments