MVUA iliyonyesha kwa zaidi ya masaa manne Machi 27 mwaka huu katika mji Iringa imesanbabisha madhara makubwa ya miundo mbinu eneo la Mkimbizi bima na baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa baada ya barabara inayounganisha kata hiyo na kata ya Mtwivila kuwa hatarini kukatika.
Wakizungumza na matukio Daima Tv wakazi wa eneo hilo Silla Kimwanga na Sara Sanga walisema kuwa mvua hizo zilianza juzi usiku na kumalizika jana asubuhi zimepelekea barabara hiyo sehemu kubwa kukatika na maji ya mvua .
Kimwamga alisema eneo hilo ambalo barabara inakaribia kukatika yote ni eneo ambalo awali wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) Manispaa ya Iringa alikuwa amejenga mtaro wa chini ya ardhi wa kupitisha maji ( karavati) ambalo mbali ya kujenga karavati hilo bado eneo hilo kuna karavati ambalo limeziba halipitishi maji hivyo kuepelekea maji kupia juu ya barabara na kuleta madhara makubwa eneo hilo .
“Kero hii ni kubwa sana kwetu wakazi wa eneo hilo na barabara hii pia inaunganisha kata ya Mtwivila na iwapo barabara eneo hilo haitafanyiwa kazi upo uwezekano mkubwa wa watumiaji wa barabara hii kwa kata ya Mkimbizi na Mtwivila kukosa mawasiliano kama watahitaji kutumia barabara hii .
Huku Sara Sanga akiomba uongozi wa TARURA Manispaa ya Iringa kutembelea maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa ili kutazama changamoto iliyotokana na mvua hizo kwani yawezekana maeneo mengine madhara ni makubwa zaidi ya hayo .
Huku diwani wa kata ya Mkimbizi Eliud Mvella akithibitisha kutokea kwa madhara hayo na kuwa eneo hilo linahitaji ufumbuzi wa haraka zaidi ya kunusuru barabara hiyo ambayo ni moja kati ya barabara muhimu sana katika kata hiyo hivyo madhara hayo ni makubwa zaidi na kutaja barabara nyingine zilizokumbwa na madhara kuwa ni pamoja na ile ya Ugele ambayo pia imekatika kutokana na mvua hizo.
Mvella alisema barabara nyingi za TARURA zimewekwa wakandarasi toka mwaka jana ila changamoto kubwa ni makandarasi kuwa na kazi nyingi za kufanya hivyo kupelekea baadhi ya kazi kuchelewa kiufanyika japo muda wa ukamilishaji wa kazi bado unawaruhusu .
MKandarasi Vitus Mushi akizungumzia tatizo la wakandarasi kuwa na kazi nyingi na kuchelewesha baadhi ya kazi alisema suala hilo halina uhalisia kwani TARURA na wakandarasi wanamikataba ya kazi muda wa kuanza na kumaliza kazi hivyo kinachofanyika na makandarasi kuzingatia muda wao wa kazi .
Naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Juli Sawani akizungumzia madhara ya mvua hizo alisema sehemu kubwa ya Manispaa ya Iringa imekubwa na madhara japo kwa sasa ni mapema kujua ukubwa wa madhara hayo kwani tathimini zinafanyika kupitia madiwani wa kata husika .
Sawani alisema kwa upande wa kata ya Mkimbizi diwani wake amekuwa mbele sana kufuatilia changamoto za miundo mbinu na kuzifanyia kazi hivyo kwa hilo la barabara kutaka kukatika ofisi yake itamjulischa meneja wa TARURA ili kupita maeneo yote korofi na kuyafanyia kazi .
Meneja wa TARURA wilaya ya Iringa Barnaba Jabiry akizungumza kwa njia ya simu na juu ya madhara ambayo TARURA imeyapata kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha alisema kuwa changamoto ni kubwa kwani mbali ya maeneo hayo zipo baadhi ya barabara zimefungwa kabisa kutokana na kukatika .
Hata hivyo alisema wanaendelea kutatua changamoto za miundo mbinu katika maeneo mbali mbali ndani ya wilaya ya Iringa ili kuona wananchi wanaendelea kupata huduma kama kawaida japo alisema kutokana na madhara hayo ya mvua kuna uharibifu mkubwa zaidi hiyo bajeti ya matengenezo ya barabara itakuwa kubwa zaidi .
0 Comments