Ujenzi wa Mradi
wa usambazaji maji katika miji mitatu ndani ya mkoa wa Iringa ambao utagharimu
dola milioni 105 unatarajiwa kukamilika mwaka 2027, huku ukiwa nauwezo wa
kusambaza maji kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa, Kilolo na Ilula, bila kikomo
mpaka mpaka mwaka 2045.
Akiongelea
mradi huo Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Peres Magiri amewataka wananchi wa maeneo
hayo kulinda chanzo hicho cha maji kutoka mto mtitu ili kuweza kufikia malengo
ya pamoja ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa maeneo yaliyokusudiwa.
“lazima kuwe
na juhudi za pamoja kwanzia kwa wadau, wananchi na serikali kwa kutoa elimu juu
ya umuhimu wa mradi huo kwani umetokana na juhudi za rais Samia Suluhu Hassan
ambaye ametafuta fedha hizo kutoka kwa watu wa Korea na mpaka 2027 mradi
utakuwa umekamilika hivyo tunamshukuru sana”.
Hata hivyo,
Dc Magiri amesema mradi huo utakwenda kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 6000 ambao
wote ni wazawa hivyo kuwataka vijana hao kuchangamkia fursa hizo ili kuondokana
na wimbi la ukosefu wa ajira.
Mhandisi
Fabian Maganga, mkurugenzi wa usambazaji maji, na menejimeti ya usafi wa
mazingira mamlaka ya maji Iringa (IRUWASA,) amesema wanatarajia kukusanya kiasi
cha lita milioni 33 kwa siku, kutoka katika Chanzo cha maji cha mto mtitu jambo
ambalo litakuwa suluhisho la upatikanaji wa maji ya uhakika na kwa gharama na
fuu, kwa miji mitatu ya Kilolo kwa asilimia 85, Ilula kwa asilimia 85 na kwa
manispaa ya Iringa ni asilimia 100.
Aidha, Mhandisi
Maganga, amaongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo, kutapunguza kilio cha wateja
wa maji kutoka mamlaka ya maji Iringa juu ya ukubwa bili ambao unatokana na matumizi
makubwa ya umeme katika usambazaji wa maji hayo hasa kwa wakazi wa manispaa ya
Iringa.
“maji
yatakayo toka katika mto mtitu yatasafiri takribani umbali wa kilomita 46 mpaka
kufika Iringa mjini kwa njia ya mtiririko ikiwa na maana ya kwenda kupunguza gharama
za kutumia umeme katika kusambaza umeme, hivyo kile kilio cha siku zote cha
bili kubwa huenda kitapata suluhisho kutokana na kupata maji kwa njia ya
mtiririko”.
0 Comments