Header Ads Widget

HALMASHAURI YA MBINGA MJI YAPONGEZWA KUFANYA VIZURI KWENYE MBIO ZA MWENGE MSIMU ULIYOPITA.

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo
Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbinga Mji  Kevin Mapunda
Mkurugenzi wa Halmashauri Mbinga mji Grace Quintene
Mtumishi wa Halmashauri ya Mbinga mji aliyeongoza kukesha na mwenge msimu uliyopita Gilbert  Gotifrio.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Amon Mtega, Mbinga.

MKUU wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Aziza Mangosongo ameipongeza Halmashauri ya Mbinga mji kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa na kikanda huku kitaifa nafasi ya 10 kwenye mbio za mwenge katika msimu uliyopita.


Pongezi hizo amezitoa kwenye kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo ambalo limekuwa na agenda moja ya kupitisha rasimu ya bajeti ambapo wamepitisha rasimu hiyo ya Sh.Bilion 25.6 ya mwaka wa fedha 2023 /2024.


Mangosongo akitoa salamu za Serikali kwenye Baraza hilo ambalo limehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda amesema kuwa Halmashauri ya Mbinga mji imeshika nafasi hiyo kwenye suala la ukimbizaji mwenge ni kutokana na mshikamano baina ya madiwani na watumishi wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na mkurugenzi Grance Quintene .


 Mkuu wa Wilaya hiyo hakusita kumuelezea mmoja wa watumishi wa Halmashauri hiyo Gilbert Gotifrio ambaye ni Afisa nyuki katika Halmashauri hiyo kuwa aliongoza katika watumishi kukimbia na Mwenge katika maeneo mbalimbali ya miradi pamoja na kukesha na Mwenge huo.


Aidha Mangosongo amewataka msimu huu wajipange tena ili kutetea nafasi hiyo ambao Mwenge huo utakimbizwa Wilayani humo Aprili 22 na 23 mwaka huu huku akimpongeza utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa katika Halmashauri hiyo jambo ambalo lina leta heshima mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akitoa fedha nyingi kwenye miradi hiyo.


Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda wakati akitoa neno la shukrani kwa mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa bila kuficha Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mingi ya kimikakati katika Wilaya hiyo hivyo Wananchi wana kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono kwenye utekelezaji huo.


Naye mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kevin Mapunda amesema Halmashauri hiyo kupitia mkurugenzi wake Grace Quintene kuwa imejipanga vema katika kuhakisha miradi yote inatekelezeka kwa wakati pamoja na kuupokea Mwenge katika msimu huu Aprili 22 na 23 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI