Header Ads Widget

WAZIRI PROF MBARAWA ASIFU UJENZI UWANJA WA NDEGE IRINGA ,MNEC ASAS AOMBA UHARAKISHAJI BARABARA YA MCHEPUKO

 


Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbalawa aliyefanya ziara katika uwanja wa ndege wa Iringa mkoani Iringa amesema ameridhishwa na maendeleo ya uwanja huo kwa hatua uliyofikia na kuwahimiza kuendelea na kasi hiyo ili kumaliza kwa wakati waliojipangia.


Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole amesema, uwanja wa ndege wa Iringa utakuwa chachu ya maendeleo nchini kupitia sekta ya utalii kwani watauunga na barabara ya kwenda Hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Naye mbunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi ameipongeza serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipa kipaumbele miradi itakayoiinua Tanzania kimaendeleo na kiuchumi.


Awali, akimkaribisha Waziri wa Ujenzi na uchukuzi, MNEC Salim Abri Asas ameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya mchepuko kutoka mikoa mingine ya nyanda za juu kusini kama njombe na mbeya ili kupunguza adha ya usafiri mkoani Iringa.

Uwanja huo uliozinduliwa Agosti mwaka jana kwa ajili ya ukarabati na upanuzi na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dakta Samia Suluhu Hassan na unaokadiliwa kukamilika Agosti mwaka huu umefikia 45% mpaka sasa na kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni 43 ikiwa ni ongezeko kutokana na upasuaji wa mwamba kutoka bilioni 21 zilizotolewa mwanzo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI