Uongozi mzima wa Simba sc umezindua wiki ya hamasa kuelekea mchezo wa Kimataifa kati ya Simba Sc dhidi ya Raja Casablanca ambao unaenda kupigwa katika uwanja wa Mkapa Stadium jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Mashabiki wa timu ya Simba sc msemaji wa timu hiyo Ahmed Ally amesema hayo kwenye Tawi la Home Boys Tegeta Jijini Dar es salaam na kusema timu ya Simba sc inahitaji ushindi Katika mchezo huo ambao unaenda kupigwa siku ya jumamosi.
"Tunatambua mchezo utakuwa mgumu na sisi kama Simba sc tunatambua umuhimu wa mchezo huo,ambao ndiyo mchezo muhimu uliobakia Tanzania kwa ujumla na yeyote anayekuja uwanja wa Benjamin Mkapa *HATOKI MTU* huku akimalizia kwa kusema yeyote anayekuja." Ahmed Ally Msemaji wa Simba Sc
Pamoja na hayo ndugu Ahmed Ally amewaomba mashabiki kujitokeza kwa winigi siku ya Jumamosi kwani mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa kiungwana,hivyo mashabiki wa Simba jitokezeni kwa wingi siku ya Jumamosi kuipa sapoti timu yenu ya Simba Sc.
Pia msemaji ameenda mbele na kusema kwamba siku hiyo kutokuwa na burudani kubwa zaidi kwa wale ambao wanapenda mzuka zaidi,Kwani mkiwahi kununua tiketi mapema inakua inakuwa rahisi zaidi kuelekea mchezo huo kwani Jumamosi timu ya Raja Casablanca wanaenda kutueleza ilikuwaje wakapata matokeo mazuri mbele yao.
Naye,Mwenyekiti wa Simba Sc Murtaza Mangungu amewashukuru mashabiki wa timu ya Simba sc kwa kuonyesha mapenzi na timu yao na kusema dhumuni letu ni kuujaza uwanja wetu wa Benjamin Mkapa,lakini pia niwatoe wasiwasi kwamba benchi na wachezaji wetu wapo timamu wapo vizuri kuelekea mchezo dhidi ya Raja Casablanca.
Lakini pia amemshukuru mhe.Rais kwa kiasi cha fedha ulizozitoa na tunajua fedha hiyo itaenda upande mmoja inabidi tu wakubali,na zaidi nitoe shukrani zangu za dhati kwa matawi yote ya Simba Sc kwa ummoja wenu huo mnaouonyesha kwa timu yenu."Amesema Murtaza Mangungu Mwenyekiti wa Simba Sc.
0 Comments