Header Ads Widget

WAZIRI NAPE AIPONGEZA TOMA


Waziri wa Habari Mhe Nape (picha ya maktaba)


Mkurugenzi wa habari maelezo na msemaji wa serikali Gerson Msigwa akiongea na waandishi wa habari pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua taasisi ya Tanzania Online Media Alliance(TOMA)kwenye ukumbi wa hotel ya Morena Dodoma

Na Editha Karlo,Matukio Daima Dodoma

Waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye ameipongeza klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha(APC)kwa kuanzisha taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni,Tanzania Online Media Alliance(TOMA).


Nape ameyasema hayo februari 10 2022 kwenye ukumbi wa Hotel ya Morena kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na msemaji wa serikali na mkurugenzi wa habari maelezo Gerson Msigwa wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo jijini Dodoma.


Waziri Nape ameutaka uongozi wa klabu ya waandishi wa habari Arusha(APC)kuendesha mafunzo ya weledi kwa waandishi wa habari mtandaoni kwa vile kwani wengi hawafuati misingi ya uandishi wa habari.


Alisema sasa hivi vyombo vingi vya habari vya mtandaoni vinasumbuliwa na weledi,baadhi uzusha habari ambazo hazipo na kuzua taharuki kwenye jamii.


"Tunapaswa kujitofautisha ili tulinde taaluma yetu na serikali ina ona juhudi za vyombo vya habari ndo maana imetoa uhuru wa kutosha kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo chake"alisema Msigwa


Aliwaomba wadau wa masuala ya habari na wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia weledi katika utendaji wa kazi zao hasa katika kipindi hiki cha matumizi ya teknolojia kwa kuhakikisha wanazingatia maudhui yanayoendana na taaluma.


Aliwataka pia waandishi wa habari za mtandaoni kujiunga kwa wingi na taasisi ya TOMA ili waweze kunufaika na taasisi hiyo pia kuwa waandishi wenye weledi katik taaluma yao.


"Nimestuka kidogo taarifa yenu imesema mnawanachama 20 tu hii imenisikitisha uchache huu Tanzania waandishi wapo wengi wanaoandika habari za mtandao niwaombe waandishi mjiuunge kwa wingi na taasisi hii"Alisema Msigwa



Naye mtendaji mkuu wa Taasisi ya Freedom House Tanzania,wakili Daniel Lema alisema kuanzishwa kwa taasisi wanahabari za mtandaoni(TOMA)ni matokeo ya mradi wa kuimarisha demokrasi nchini(DataDriven Advocacy)ambao ulikuwa chini ya ofisi yake na shirika la pact.


Alisema mradi huo ulikuwa ukifanywa na kusimamiwa na chama cha waandishi wa habari Arusha(APC)ambao umeleta manufaa makubwa kwa waandishi 20 waliokuwa wakitekeleza mradi huo ambapo wameweza kupatiwa mafunzo mbalimbali yanayoendama na taaluma yao pia baadhi yao wameweza kumiliki vyombo vyao ya mtandaoni,wengine wakipewa tunzo na serikali kwa kutambua kazi zao.

Naye Mwenyekiti wa Arusha Press Club ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya TOMA Claud Gwandu alisema taasisi hiyo imeanzishwa baada ya kuona uandishi wa mitandaoni unakua kwa kasi japo baadhi wanaripoti taarifa ambazo hazina weledi.


"Tumefungua milango ipo wazi wanachama wengi waje kujiung na TOMA,tutahakikisha taasisi yetu inakuwa na waandishi wenye weledi katika uandishi wao,tutawapa mafunzo ili kuwajengea uwezo kwenye kazi zao "Alisema Gwandu


Mtendaji wa taasisi ya TOMA(aliyeshika maiki)Seif Mangwangi akitoa maelezo kuhusu mtandao wa TOMA uliozinduliwa na msemaji wa serikali

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI