Header Ads Widget

WATU WANNE MBARONI KWA KOSA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI






NA, TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima Kagera.

JESHI la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu kwa kutumia kikosi cha askari wa hifadhi za Taifa Ibanda-Kyerwa na Rumanyika-Karagwe limefanikiwa  kuwakamata majangili wanne wakiwa na nyara za serikali ikiwemo meno ya Tambo yenye uzito wa kilogram 9.15.


Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Hifadhi ya Taifa Ibanda-kerwa, ACC Frederick M.Mofulu  amesema kuwa majangili hao walikamatwa mnamo Februari 3 mwaka huu majira ya saa tatu husiku Katika Kijiji cha Muungano na Lusaunga wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.


"Majangili hawa wamekamatwa wakiwa na nyara za serikali ikiwemo meno mawili ya Tambo,ngozi ya fish,kichwa cha fisi, vipande vitatu vya ngozi ya nyati, mkia wa nyati, ngozi ya swala pala lakini pia walikutwa na silaha mbili aina ya gobore pamoja na risasi tatu za kienyeji aina ya gololi ambazo hutumika kwa ajili ya kuua wanyama"


Aidha amesema kuwa baada ya majangili hao kukamatwa na kikosi cha askari wa jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu (TANAPA) walishirikiana na jeshi la polisi wilaya ya Biharamulo katika hatua mbalimbali zilizofuata.


"Majangili walikamatwa nipamoja na Raphael Daud(44), Fikiri Simon Lugaira(43), Majaliwa Isaya Charles(42) na Warwa Budura Rupilya(45), wote wakiwa ni wakazi wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera"


Sambamba na hilo, Kamanda huyo ametoa rai kwa watanzania wote kutojihusisha na vitendo vya ujangili dhidi ya maliasili kwani jeshi la Polisi  liko imara na kwamba yeyote atayejihusisha na vitendo vya ujangili atakamatwa na kuchuliwa hatua Kali za Kisheria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI