Na Pamela Mollel,Kitulo
Wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi ya Taifa Kitulo wametakiwa kuheshimu na kutunza vyanzo vya maji ikiwemo kuzingatia mita 60 iliyowekwa na serikali ili kuepuka shughuli za kibinadamu kuathiri maeneo hayo muhimu
Akizungumza katika hifadhi hiyo ya Kitulo eneo la usalama lenye maporomoko makubwa ya maji ,Afisa Mhifadhi Paschal Makumbule alisema kuwa uwepo wa maji katika eneo hilo ni muhimu sana kwakuwa inasaidia wanyama na kustawisha mimea
Alisema wananchi wanaozunguka eneo la vyanzo vya maji katika hifadhi wanatakiwa kutunza mazingira ya eneo hilo ili kuendelea kubaki katika uhalisi wake
Alitaja umuhimu mwingine wa kutunza eneo hilo kuwa maji yanayopatikana katika chanzo hicho husaidia kuzalisha umeme ambapo maji hayo hutiririka kuelekea mto Mtera hadi bwawa la Nyerere ambao ni mradi mkubwa wa Taifa
"Bado tunaendelea kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji sambamba na utunzaji wa mazingira kwa ujumla ili kuepuka kuharibifu wa mazingira kwa ujumla "alisema Makumbule
Alisema uwepo wa vyanzo vya maji ni muhimu sanaa kwa Taifa zima ikiwemo wanyama na mimea
Kwa upande wake Afisa Utalii Tanapa Mohammed Kiganja aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kutembea vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi ya Kitulo na kujionea maporomoko makubwa ya maji
"Uwepo wa maji haya inasaidia sanaaa katika uzalishaji wa umeme wa Taifa,shughuli za kilimo na ufugaji hivyo tuendelee kutunza vyanzo vya maji "alisema Kiganja
0 Comments