Header Ads Widget

WAKUU WA WILAYA WAPYA KILIMANJARO WAAPISHWA.

 


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amewaapisha wakuu wa wilaya wapya watatu wa Wilaya za Zame, Siha na Hai Walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Walioapishwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni, Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt.Christopher David na Amir Mohammed mkuu wa Wilaya ya Hai.



Mkuu huyo wa mkoa amewataka viongozi hao wapya kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyao, pia kutambua kuwa wajibu wao ni kusikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi.



"Nimesha pata fununu kuhusu migogoro iliyopo kule Same hasa ya ardhi na suala hilo ndilo nitaanza nalo".Kasilda Mgeni baada ya kiapo kuwa mkuu wa Wilaya ya Same.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS