Imeelezwa kuwa matatizo mengi ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto yanaendelea kuongezeka katika jamii na hivyo kusababisha wadau wa maendeleo katika manispaa ya moshi kukutana na Kujadili ni jinsi gani wanaweza ya kuweza kushirikiana na kutokomeza ukatili wa Kijinsia.
Hayo yameelezwa na Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Moshi Bi.Magreth Ruben wakati alipokuwa katika kikao cha wadau wa maendeleo ambao ni watendaji wa kata waalimu wa shule za msingi na Sekondary iliyofanyika Wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambayo yameandaliwa na shirika la Simba Footprint.
Amesema kuwa wazazi na walezi Wana majukumu ambayo wanatakiwa kuyajenga kwa ajili ya kizazi kinaachokika ambapo wanatakiwa kuanza kuanzia sasa kwa watoto wanaoishi nao kwa kuwafundisha kuwa kuna ukatili wa kijinsia unaoendelea katika jamii.
"Kwamba tutengeneze malezi ya watoto na kuwaonesha kwamba watoto wote wana haki sawa na wanatakiwa wakuzwe katika usawa wa kupata haki zao za msingi na kutimiza wajibu wao na pia kuhakikisha mazingira wanayoishi ni salama na wanalindwa"
Hata amewataka wazazi na walezi kutenga Muda wa kuukaaa na kuwaleta karibu ili waweze kueleza yale ambayo yanapenda na yale ambayo yanawachukiza kwani bila kufanya hivyo wazazi watajikuta watoto wao wameingia katika dimbi la ukatili bila wao kujua.
Kwa upande wake belinda Urio kutoka katika shirika hilo lisilo la Kiserikali la Simba Footprint amesema wazazi na walezi wanapowapuuza watoto watajina kwamba hawadhaminiki jambo ambalo sio sahihi na hiyo inafanya ukatili wa watoto kuendelea.
" Kumbe ungeliskiliza labda mtoto amekuwambia alikuwa anatembea barabarani kuna mtu akarusha jiwe bahati mbaya halikumpiga wewe hukumsikiliza saa hiyo basi ujue kuna siku lile jiwe litampiga.
Kwa mujibu afisa ustawi wa jamaii amesema kuwa hali ya ukatili wa kijinsia katika manisapaa ya moshi harishishi lakini wanaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari pamoja na kufany mikutano kwa wananchi.
"Kwa mfano tukiangalia katika mfumo wetu wa taarifa kwa mwezi wa 10,11 na 12 ambayo ni robo ya utekelezaji , katika manispaa ya Moshi Tunaona Kwamba ukatili uliyofanyika ulikuwepo ni elfu moja mia saba na tatu, ambapo tunaona kwamba ukatili wa kimwili matukio ni Mia tatu na kumi na tano, ukatili wa kingino matukio ni mia moja sitini na nane na ukatili wa kihisia ni matukio ya wanawake 593 wanaume 109.
Kwa upande wao washiriki walioshiriki katika kikao hicho akiwwmo mwenyekiti wa Dawati la kata ya miembeni Agnes Kambi amesema kuwa suala la kulawitiwa kwa watoto ni suala ambalo linafanya jamiii kutoa machozi kila mara.
"Lakini kwa hii semina tuliyoipata imetusaidia sana kufungua Macho na tukaona kwamba ukatili sio kulawitiwa peke yake bali kuna ukatili wa aina nyingi kama ukatili wa kipigo kwa wanawake na wanaume, lakini pia ukatili wa maneno yaani elimu ya leo imetufanya tujue mambo mengi sana kwani kuna watu wanofanya ukati lakini hawajui kwamba wanafanya ukatili" Alisema.
0 Comments