Na Pamela Mollel,Kitulo
Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ni hifadhi pekee iliyojaliwa utajiri mkubwa wa maua pamoja na ndege wenye uwezo wa kuruka kutoka Bara moja hadi jingine
Kutoka na upekee wake hifadhi hii hujulikana zaidi kama"Bustani ya Mungu "hii ni kutoka tu na eneo hilo kupambwa na aina mbalimbali za maua mazuri yakuvutia yenye rangi nzurii na harufu ya kipekee
Hifadhi hii inapatikana Nyanda za juu kusini mwa Tanzania katika Mikoa ya Mbeya na Njombe ikiwa na ukubwa wa kilomita za Mramba 412.9
Akizungumza na waandishi wa habari za Uhifadhi Afisa Mhifadhi katika hifadhi hiyo Paschal Makumbule anasema spichi zaidi ya 350 za maua zinapatikana katika eneo hilo huku aina 40 za maua hazipatikani popote duniani
"Uwepo wa maua katika hifadhi hii unajiuza sanaaa watu kutoka pande zote za dunia hutembelea eneo hili kwaajili tu ya kujionea maua yanayopatikana hapa"alisema Makumbule
Alisema maua katika hifadhi hiyo huchanua vizuri kwa rangi tofauti kipindi cha masika na eneo hilo limepewa jina Bustani ya Mungu kwa kuwa hakuna mtu aliyepanda hayo maua wala kupalilia au kuangalia kwa namna yeyote isipokuwa maajabu ya Mungu
Mbali na uwepo wa maua pia kuna ndege wengi wanaopatikana katika hifadhi hiyo wenye uwezo wa kuruka kutoka Bara moja hadi jingine
Inasemekana Ndege aina ya Tandawili machaka ni ndege wa ajabu sanaaa kwa namna ambavyo anaweza kutaga mayai na kuzaliana kwa wingi kabla ya kwenda mabara mengine
Hifadhi ya Kitulo inapambwa pia na uwanda wa tambarare ,Mabonde,Vilima na maporomoko makubwa ya maji pamoja na mabwawa ambayo ni muhimu sana kwa ustawi mto Ruaha Mkuu ambao ni tegemezi kwa hifadhi ya Ruaha
Kutokana na upekee wake wanakaribishwa watu mbalimbali wenye matukio yao muhimu kama vile harusi,Valentine day kufanya matukio hayo katika hifadhi ya Kitulo iliyojaliwa maua mazuri na yakuvutia yenye upee wa aina yake
Hifadhi ya Taifa Kitulo ilianzishwa mwaka 2002 na kutangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa na serikali mwaka 2005
0 Comments