NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ameitaka jamii kutowanyanyapaa watoto wenye ulemavu wa aina yeyote ile na kuwaona hawafai kupelekwa shule ili kuweza kupata haki yao ya Msingi.
Hayo ameyabainisha katika maadhimisho ya siku ya Braille yaliyofanyika Kitaifa Mkoani hapa na kueleza kuwa watoto hao wanahaki ya kusoma kama watoto wengine wasio kuwa na ulemavu.
Malima ameeleza kuwa serikali Kwa kushirikiana na wadau mablimbali Kwa kutambua umuhimu wa watu wenye ulemavu hususani wasioona wameweza kuwapa vifaa vya kujifunzia pamoja na kutoa mahitaji mengine muhimu.
Ameeleza kuwa mwaka 2022 watoto 2883 wenye ulemavu waliweza kujiunga na elimu ya awali na 3318 walipata nafasi ya kujiunga na elimu ya Msingi huku 1157 wakiwa wamejiunga na kidato Cha kwanza.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu wameweza kutoa ajira Kwa walimu wenye ulemavu 261 huku kati ya hao 61wakiwa ni walemavu wasioona na wengine 14 wasioona wamepata kazi katika sekta ya afya.
"Hawa ni watoto wa Kitanzania wenye ulemavu waliopata nafasi za ajira na shule Kwa hiyo isitokeee mtu yeyote mwenye Mtoto mwenye ulemavu akasema huyo hafai kwenda shule wote wana nafasi ya kusoma" Alisema Malima.
Aidha Kwa upande mwingine amelweza kuwa imetengeneza muongozo wa kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalumu kufikia malengo huku ikiwa inalenga kuboresha miundombinu inayojielekeza kuwahudumia walemavu wakiwa mashuleni.
Mwenyekiti wa Jumuiya wasioona Tanzania (TAB) Omary Itambu ameeleza kuwa jamii kutambua kuwa kupata Mtoto mwenye ulemavu sio mkosi Wala nuksi ni baraka Ndani ya Nyumba.
Itambu ameeleza kuwa ukipata Mtoto mwenye ulemavu wa aina yeyote ni lazima kumpeleka shule kwani siku hizi hakuna kinachoshindikana mzazi asipompeleka Mtoto shule atakuwa amemnyima haki yake ya Msingi .
" Na mzazi atakuwa amechangia kusema Yale maneno yasemwayo Nina mzigo nyumbani kwangu kumbe umeyata mwenyewe" Alisema Itambu.
Ameeleza kuwa Maadhimisho ya Breile yamekuna kuleta mageuzi makubwa Kwa watu wasioona na kuiomba serikali kutoka katika Mfumo wa analojia na kwenda katika Mfumo wa kisasa kidigital kwani Mfumo huu unatumia gharama kidogo kuliko huo wa zamani.
" Maandishi haya yamekuna kutoa gizani sisi tulikuwa wafungwa, sio wafungwa wa gerezani ni wafungwa wa maarifa na elimu na baada ya maandishi haya kuja na sisi tumepata msamaha wa Rais Kwa maana ya kuingia darasani" Alisema Itambu.
Mkurugenzi wa Desk anda Chair foundation Sibtain Meghee ambaye pia ni mdau ameeleza kuwa Kuna haja ya kuboresha upatikanaji wa vifaa Kwa njia rahisi ili kuweza kuwafikia walengwa Kwa wepesi.
Ikumbukwe kuwa mgunduzi wa maandishi Hayo Luis Breile alizaliwa mnamo mwaka 1809 huku ufaransa na alipata ulemavu wa macho akiwa na umari wa miaka mitatu (3) katika kiwanda Cha baba ake Cha kutengeneza ngozi Kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
0 Comments