Header Ads Widget

MBUNGE PROF NDAKIDEMI AIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI MASOKA.



Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Profesa Patrick Ndakidemi ameahidi kukabidhi madawati 25 pamoja na fedha taslim laki nane kusaidia katika ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya Sekondari Masoka.


Prof. Ndakidemi alitoa ahadi hiyo jana wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Masoka iliyopo Kata ya Kibosho Kirima katika jimbo la Moshi vijijini kwa mwaka 2023.



Akiwakaribisha wazazi, Mkuu wa shule Ahmed Litinji alieleza kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa za upungufu wa madarasa, upungufu wa maabara, upungufu wa matundu 14 ya vyoo,  uhaba wa waalimu wa masomo ya kilimo, biolojia na kemia, uhaba wa samani za ofisi na uhaba wa madawati. 

Mbunge aliongoza harambee ambapo wadau wa maendeleo wa shule ya Masoka walichangia saruji na fedha Milioni mbili ili kutatua changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo.



Katika hafla hiyo, mbunge Ndakidemi alitoa zawadi kwa waalimu na wanafunzi waliofanya vizuri na aliwaahidi walimu wa Masoka kuwa atawakaribisha kula chakula cha mchana naye akitambua juhudi zao zilizoifanya shule hiyo iwe ya pili kwa ubora kwa shule za serikali katika Halimashauri ya Moshi. 


Hafla hiyo ilihudhuriwa na wazazi, viongozi wa dini mbalimbali, na wanakijiji kutoka katika kata ya Kibosho Kirima na ilipambwa na aina tofauti za burudani kutoka kwa wanafunzi waliojaliwa kuonyesha vipaji vyao ikiwemo kutoa mafunzo kwa wananchi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwa lugha fasaha za kiingereza na kiswahili.


Wazazi walioshuhudia burudani hizi kutoka kwa watoto wao waliamua kuwazawadia fedha wakionyesha hisia za kufurahi.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI