Header Ads Widget

PROF. MBARAWA MGENI RASMI HAFLA YA UTIAJI WA SAINI BARABARA YA LUSAUNGA, RUSUMO.

 


Na Titus Mwombeki, Matukio Daima App Kagera.


WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkandarasi wa Ujenzi wa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Benaco Ngara mkoani Kagera.


Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa hafla hiyo itafanyika Februari 18 mwaka huu eneo ya Benaco Ngara.


 "Rais Dkt. Samia Suluhu ameruhusu na kuidhinisha fedha za ukarabati na kujenga upya barabara ya Lusaunga- Lusumo(92km) chini ya mpango wa ushirikiano wa usafiri Tanzania, katika hafla hii tunategemea prof.Makame Mbarawa, waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuwa mgeni rasmi"



Ameongeza kuwa kwakutambua umuhimu wa barabara hiyo inayounganisha nchi ya  Tanzania, Rwanda na Burundi Dkt.Samia Suluhu Hassan ameona sasa ndiyo muda muafaka wa kufungua uchumi wa mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla kwa kupunguza vikwazo vya barabara chakavu mkoani humo.


Sambamba na hilo, Chalamila amesisitiza kuwa pamoja na utiaji wa saini wa mkataba huo,  mkoani Kagera kuna miradi mikubwa ya Maendeleo ambayo ipo katika hatua za manunuzi na kusaka mkandarasi ikiwa ni pamoja na Omugakorongo kuelekea Kigarama mpaka Murongo, Bugene kuelekea Kaisho mpaka Morongo, Kagera Sugar Junction(Bunazi) kuelekea kitengule.


Aidha amewasisitiza wananchii pamoja  na wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kushuhudia hafla hiyo ya utiaji wa saini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI