Header Ads Widget

MBUNGE SEMUGURUKA ATOA PIKIPIKI KWA MAKATIBU UWT KAGERA







NA, TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera 


MBUNGE viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Oliver Semuguruka ametoa pikipiki nane kwa makatibu wote wa UWT mkoani kagera kwa lengo la kukijenga Chama .


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi pikipiki hizo aina ya Boxer kwa makatibu hao amewasisitiza kuzitumia pikipiki hizo kuwafikia wananchama ambao wako sehemu ambazo zilikuwa hazikiki kirahisi.


"Kama mnavyojua jiografia ya mkoa wetu ilivyo ni mabonde na milima kwa wingi, kutokana na changamoto hiyo mimi kama mbunge  nimewiwa kutoa pikipiki hizi kwa  viongozi hawa ziwasaidie katika ujenzi wa CCM ikiwa ni pamoja na kuwafikia wananchi katika maeneo ya ndani kabisa vijijini ambayo ayafikiki kirahisi ili wapate kusajiliwa"


Aidha, amewasihi viongozi hao kutambua kuwa kipindi hiki ni kipindi muhimu hasa katika kukijenaga chama kwa kufanya usajili wa wanachama wapya kwani uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa vijiji na mtaa unakaribia.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa humo, Hajati Faidha Kainamula amemshukuru mbunge huyo kwa kutoa pikipiki hizo kwa makatibu wote ambao ndio watendaji wakuu huku akiwasisitiza makatibu  hao kutumia vyombo hivyo vya usafiri  ipasavyo ili kufanikisha lengo kusudiwa.


"Hawa ndio aina ya wabunge ambao tumekuwa tukiwataka katika mkoa wetu, kwakweli tunashukuru sana mbunge wetu Oliver Semuguruka kwa kuona changamoto iliyokuwa ikitukabili na kuitatua na nimuakikishie kuwa pikipiki hizi zitakuwa salama na zitafanya kazi kusudiwa kwa uangalizi wa karibu kutoka kwetu viongozi wote wa UWT mkoani Kagera"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI