Header Ads Widget

MWENYEKITI UVCCM MWANGA AISHA MFAUME AJITOSA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII MWANGA..

 


AITA WAWEKEZAJI WA UTALII 


NA WILLIUM PAUL, MWANGA.

UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wamewaomba wawekezaji wa utalii kwenda kuwekeza katika wilaya hiyo kwani inafursa mbalimbali za utalii.



Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mwanga, Aisha Mfaume alipofanya ziara kujionea vivutio vinavyopatika katika wilaya hiyo ambavyo ni misitu ya asili, ziwa jipe, mapango ya kale, maeneo ambayo yalikuwa yakitupiwa watoto waliokuwa wakianza kuota meno ya juu yajulikanayo kama Mkumbavana pamoja na bwawa la Nyumba ya Mungu.


Aisha alisema kuwa, wilaya ya Mwanga inavivutio vingi vya utalii lakini tatizo ni utangazwaji wa vivutio hivyo ikiwemo milima na kuwaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kufika kujionea vivutio hivyo na kuweza kuwekeza.



"Wilaya ya Mwanga tunavivutio vingi vya utalii lakini vimekuwa havitangazwi hivyo sisi kama Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi tumeamua kujitoa kuvitangaza vivutio hivi ambavyo vitatuingizia kipato kwa wilaya yetu pamoja na vijana kupata ajira za kudumu" alisema Aisha.



Mwenyekiti alisema kuwa, Rais Dkt Samia Suluhu Hasani ameonyesha juhudi ya kutangaza vivutio vya utalii nchini kupitia filamu ya The Tanzania Royal Tours hivyo wao kama Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mwanga wameamua kumuunga mkono kwa kuionyesha jamii vivutio vinavyopatikana Mwanga.



Aisha alisema kuwa, kutambulika kwa vivutio hivyo vya Mwanga vitasaidia Halmashauri kujipatia mapato kupitia Kodi lakini pia itasaidia kuponguza tatizo la ajira kwa vijana kwani watapata fursa ya kuongoza watalii huku wananchi wengine wakiuza bidhaa mbalimbali kwa watalii.


"Wilaya ya Mwanga inahistoria nyingi ambazo hazijatangazwa wawekezaji mbalimbali wa sekta ya Utalii sasa muda umefika kuja kuwekeza katika wilaya yetu na sisi kama Umoja wa vijana tunawaahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika hili" alisema Aisha.



Kwa upande wa wananchi, Ramadhani Mmbaga alisema kuwa, mbali na milima na mapango yanayopatikana katika wilaya ya Mwanga ipo pia misitu mikubwa ya asili yenye historia mbalimbali.



"Huku kwetu ugweno ipo misitu ya koo ambapo inahistoria zake na madhari inayovutia kwa wageni na wazawa kuja kutembelea na kujifunza jinsi kabila ya Wapare walivyokuwa wakiishi kwa upendo" alisema Mmbaga.



Naye Mwanaamina Juma mkazi wa Nyumba ya Mungu alisema kuwa, katika eneo hilo kunapatikana utalii wa uvuvi wa samaki lakini pia yapo maeneokwa ajili ya kujenga mapumzikio ya watalii.



"Pembezoni mwa bwawa la Nyumba ya Mungu kunaweza kuwekezwa maeneo maalum kwa ajili ya watalii kupumzika na kujionea shughuli za utalii zinavyofanyika hivyo niwaombe wawekezaji kuja kuwekeza" alisema Mwanaamina.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI