Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Said Rubbeya ameibua hoja kutoka na kero kubwa inayosababishwa na kuongezeka kwa Wizi wa kutumia Bodaboda mkoani Iringa. Ambapo amesema mbali na kuwepo na vitendo vya kiharifu na makosa ya Jinai ndani ya Manispaa ya Iringa kuongezeka kutokana na malalamiko na sio kitakwimu, wizi wa kutumia bodaboda umeongezeka kwa kasi sana na Polisi wanashindwa kudhibiti suala hili kutoka na na kukosa Ushirikiano Mkubwa na vitendea kazi bora.
Akizungumza wakati wa kuibua hoja juu ya ulinzi na Usalama kwenye Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya wilaya ya Iringa wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica Kessy, mkutano uliohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kidini amefunguka na kusema,
"Mbali na kuwepo kwa wizi mdogo mdogo lakini kitendo kilichoongezeka sana ni cha wizi unaotumia Bodaboda kitu ambacho ni kero sana haswa kwa watu wanaokaa maeneo ya Gangilonga, Kitwiru, Ruaha, Kihesa na kwingineko hii ni kero kubwa sana"
"Sis sote tunafahamu kuwa jukumu la ulinzi ni la kwetu sisi kama raia lakini Polisi wanahusika zaidi, polisi wanazo Changamoto kadhaa zinawakabili kufanya kazi hii ngumu moja ni vitendea kazi mbili rasilimali fedha lakini tatu ongezeko la watu ambapo hali hii inafanya ugumu katika kudhibiti vitendo hivi vya uhalifu"
Alimaliza kwa Kupendekeza Serikali kuwatumia zaidi Viongozi wa Mitaa hasa Mabalozi wa Nyumba 10, akitolea mfano namna ambavyo enzi za utawala wa Rais wa awamu ya kwanza JK Nyerere walivyowatumia mabalozi, walikuwa na mikakati mizuri wageni hawaingii na hawatoki bila balozi kufahamu, vitendo vya uhalifu vikitokea balozi kazi yake ni kuripoti na hatua inachukuliwa haraka. Hivyo swala la Mabalozi lipewe Kipaumbele kwani tukidumisha amani na usalama kwenye Mji wetu hata kipato kitaongezeka. Alisema Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Said Rubbeya.
0 Comments