Header Ads Widget

e-GA KUWA NA SEHEMU MOJA AMBAYO HUDUMA MTANDAO ZITAKUWA ZINAPATIKANA.

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


KATIKA kuhakikisha inajengwa Serikali ya Kidijiti, kwa muda wa kipindi cha miaka 10 ijayo, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imeendelea kutekeleza mikakati madhubuti ili kuimarisha zaidi utekelezaji wa jitihada za Serikali

Mtandao kwa kuwa na Sehemu moja ambayo huduma mtandao zote zitakuwa zinapatikana 


Akiongea leo jijini hapa wakati akiwaelezea waandishi wa habari utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo Mkurugenzi Mkuu wa e- GA Mhandisi Benedict Ndomba amesema jitihada nyingine nikuwa na uwezo wa kutumia teknolojia mpya zinazoibuka, hasa zile za akili bandia, sarafu za kidijiti na teknolojia za kifedha, ili kuwezesha maboresho ya kiutendaji katika Taasisiza Umma na utoaji wa huduma kwa Umma.


"Jitihada nyingine ni kwa vijana wa kitanzania wenye uwezo mkubwa wa ubunifu katika utekelezaji wa jitihada za Serikali mtandao kuzalisha  vifaa na miundombinu ya TEHAMA (Hardware) ndani ya Tanzania kwa kuweka Mifumo na miundombinu ya Serikali mtandao iliyo bora na imara zaidi," amesema Mkurugenzi huyo Ndomba


Aidha Amesema hadi Januari, 2023, jumla ya miradi 340 ya TEHAMA ya Taasisi za umma imepitiwa na kuthibitishwa.


"Hadi Januari, 2023, Taasisi mbalimbali za Umma zimewezeshwa kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao kwa kutoa mafunzo mbalimbali," Amesema Mhandisi upNdomba.


Hata hivyo baadhi ya mafunzo ni  usimamizi wa Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali kwa Taasisi 240, kutoa mafunzo ya mfumo wa baruapepe kwa taasisi 611 na kutoa mafunzo ya usimamizi wa tovuti kwa taasisi 492.


Mkurugenzi huyo ameeleza Mamlaka ya Serikali mtandao (e -GA ) inashirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, zikiwemo Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti, Sekta binafsi pamoja na kuandaa Vikao Kazi vya mwaka vya Serikali Mtandao ili kuwakutanisha wadau mbalimbali ambapo katika kikao kazi kilichofanyika Februari mwaka huu, jumla ya washiriki 1,624 walihudhuria.


Aidha, Mamlaka inashirikiana na Wakala ya Serikali Mtandao Zanzibar (eGAZ) kwa lengo la kuhakikisha Serikali Mtandao inaimarika kote Bara na Visiwani. Kupitia ushirikiano huu, Mifumo kadhaa imeboreshwa na inatumiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).



BAADHI YA MAENEO YA VIPAUMBELE VYA eGA


Kuendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa Taasisi zote za umma, ikiwa ni pamoja na kupitia na kukagua miradi na Mifumo ya TEHAMA ya kimkakati, kisekta na kitaasisi.


Kupitia na kutathmini hali ya usalama wa mifumo na miundombinu ya Serikali Mtandao na kuzishauri Taasisi za Umma katika maeneo ya kuboresha, pamoja na kufuatilia utekelezaji wake.


Kuendelea kuunganisha Mifumo ya Taasisi za Umma kwenye Mfumo wa Serikali wa Kubadilishana Taarifa (Government Enterprise Service Bus - GovESB).


Kuendeleza shughuli za tafiti na ubunifu katika matumizi ya teknolojia mpya za TEHAMA ili kuibua huduma mpya kwa umma na kuwezesha matumizi sahihi ya teknolojia mpya zinazoibuka.


Kujenga mifumo tumizi ya Kisekta kwa kushirikiana na Sekta husika na kuiwezesha kubadilishana taarifa na mifumo ya sekta nyingine pale inapohitajika.


Kipaumbele kingine kupanua uwezo wa Mtandao wa Mawasiliano Serikalini na kuufikisha katika wilaya zote nchini ili kurahisisha utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao na kuwafikishia huduma wananchi wote popote walipo.


Amesema Kipaumbele kingine kupitia mradi wa Tanzania ya kidijitali, wilaya zote zitaunganishwa na mtandao wa Serikali na zitakuwa na uwezo wa kufanya shughuli zao kupitia mtandao.Mradi huu upo katika hatua za manunuzi na tunatarajia ndani ya miezi 18 hadi 24 hali za halmashauri kimtandao zitaboreka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI