NA.THABIT MADAI,ZANZIBAR- MATUKIO DAIMA APP
CHAMA Chama Mapinduzi CCM Zanzibar,kimesema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameonesha uwezo mkubwa katika kulitumikia taifa na kuimarisha uhusiano wa kimataifa.
Tamko hilo limetolewa na Katibu wa Idara ya itikadi, uenezi na habari Khamis Mbeto Khamis wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu za chama hicho, kuhusu miaka miwili ya uongozi wa mama Samia kushika wadhifa huo.
chini ya uongozi wake waanchi wameshuhudia miradi mikubwa katika sekta ya afya, elimu pamoja kupunguza gharama za pembejeo kwa wakulima jambo ambalo litaongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini
Akizungumzia maendeleo yaliopatikana Zanzibar tangu Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi kushika wadhifa huo, amesema miradi mingi ya kimaendeleo imekuwa ikichomoza katika sekta ya afya, elimu, uvuvi pamoja na kufanikiwa kuimarisha misinngi ya utawlaa bora kwa kupambana na ubadhilifu na ufisadi wa mali za umma.
Serikali ya awamu ya nane imeibua mjadala mkubwa Zanzibar kutokana na miradi ya maendeleo inayoendelea kujitokeza na kubadilisha sura ya muonekano ya visiwa vya Unguja na Pemba tangu Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kukabidhiwa wazifa huo mwaka 2020.
0 Comments