Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe.Angellah Kairuki amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA. Amos Makalla kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya jijini humo ikiwemo kuratibu vizuri shughuli za Machinga.
Waziri Kairuki ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo ambapo Atembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye majimbo ya Ukonga, Segerea na Kigamboni.
Kabla ya kuanza kwa ziara,Waziri Kairuki amepokea taarifa ya utendaji kazi wa Mkoa ikiwemo Sekta ya Afya, Maji, Elimu, Miundombinu, Nishati mkataba wa lishe, Usafi wa Mazingira na vinginevyo.
Katika mazungumzo hayo RC Makalla ameelezea changamoto ya Kukosekana kwa ofisini ya Mkuu wa Mkoa ambapo Waziri Kairuki Ameahidi kufanyia kazi suala Hilo Ili Mkoa uwe na ofisi.
Pamoja na hayo Waziri Kairuki ameelekeza Halmashauri kusimamia kukamilika makusanyo ya mapato, kudhibiti madanguro, ukatili wa kijinsia, Vibali vya ujenzi, migogoro ya ardhi na kusimamia suala la lishe.
0 Comments