Header Ads Widget

DKT.MOHAMED AZUNGUMZA NA BARAZA LA WAZEE.



NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed, ameahidi kufuata ushauri,maoni na maelekezo ya wazee ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

 

Ahadi hiyo ameitoa wakati akizungumza na Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar hapo Afisini kwao Kisiwandui Unguja.

 

Alisema wazee ni kundi muhimu katika ustawi na uimara wa Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia Siasa na sera zenye tija kwa wananchi.

 

Dkt Mohamed alieleza kuwa wazee hao ambao ni Viongozi wa zamani waliohudumu chini ya Chama Cha Afro-Shiraz Party (ASP), na wakafanikiwa kuikomboa nchi kutoka katika mikono ya utawala wa kigeni.

 

"Wazee wangu nakuombeni sana mnishauri na kutoa maoni yenu wakati wowote kwani naamini Chama na Serikali zake mnazijua vizuri.

 

Pia nakuahidi kuwa  nitaumia muda,uwezo na maarifa yangu kuhakikisha Chama kinabaki salama  na kila Mwanachama anajivunia kuwa katika CCM.".Alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI